Agentina waandamana kutetea wanawake
Moja ya maandamano nchini Argentina
Maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Argentine - Buenos Aires kupinga mateso dhidi ya mwanamke .
Maandamano
hayo yamefuatia mfulurizo wa visa vya mauaji yaliyoshtua taifa hilo ,
yakiwemo yale ya mwalimu wa chekechea ambaye bwana yake alimkata koo
mbele ya darasa lake .
Vyama vya wafanyakazi , vyama vya kisiasa na kanisa katoliki wameunga mkono maandamano hayo .
Argentina imepitisha sheria dhidi ya unyanyasaji wa nyumbani, lanini wanaharakati wanasema kuwa hazitekelezwi ipasavyo .
Maandamano ya watu wachache pia yamefnyika katika nchi jirani za Chile na Uruguay.CHANZO:BBC (Muro)
No comments:
Post a Comment