Tukio la Mauaji ndani ya Kanisa la watu weusi Marekani… (Picha)

Wahusika wa masuala ya usalama wamesema 
huenda ni chuki na hasira tu za mtu binafsi zilizofanya kutokea kwa 
tukio hilo, watu walikuwa wanasali Emanuel AME Church, Charleston Marekani, akatokea mtu mmoja akafyatua risasi kwa watu waliokuwa wanasali.
Watu tisa wamefariki, bado hakuna 
taarifa rasmi kuhusu idadi ya watu wote waliokuwemo ndani ya Kanisa 
hilo… Mtu anayetuhumiwa kwa mauaji hayo ni kijana ambaye anakadiriwa 
kuwa na umri wa miaka 20 hivi.
Tukio limetokea usiku wa kuamkia leo June 18 2015, Jimbo la Carolina Marekani.
Kanisa la Emanuel AME Church ni Kanisa la Kihistoria ambalo lilijengwa mwaka 1816 ambapo watu wengi wanaosali humo mpaka leo ni Wamarekani weusi.
Jeb Bush ambaye ni Mgombea Urais wa Marekani ameahirisha kufanya Kampeni zake Charleston baada ya kutokea kwa tukio hilo.

Mmoja wa waumini amepiga magoti nje ya Jengo la Kanisa, pembeni kuna gari za Polisi ambao wamelizunguka Jengo hilo.




No comments:
Post a Comment