Dunia yatazama Wakimbizi Nyarugusu, wa Mtabila warejea tena

Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, Sospeter Christopher
 Boyo (aliyesimama mwenye shati la kitenge) akisoma taarifa fupi ya 
Kambi ya Nyarugusu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe
 (aliyeketi mwenye suti ya kijivu) aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa 
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la 
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez
 mara baada ya kuwasili kwenye kambi hiyo kujionea hali halisi ya 
mazingira na changamoto zinazowakabili Waomba hifadhi wa Burundi na 
Kongo. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Modewjiblog team, Kigoma
WAKATI
 dunia kupitia Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanahangika kutanzua 
changamoto za wakimbizi Nyarugusu, mkoani Kigoma imeelezwa kuwa idadi 
kubwa ya Wakimbizi waliorejeshwa nchini Burundi
 kutoka kambi ya Mtabila iliyoko Kigoma iliyofungwa rasmi Desemba, 2012 
wameingia tena nchini na kujazana katika makazi ya muda ya Nyarugusu 
wakiomba hifadhi.
Kauli
 hiyo imetolewa na Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu Sospter Christopher wakati
 akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi aliyekwenda kuangalia 
hali halisi ya kambi ya Nyarugusu na Wakimbizi akiambatana na Maofisa wa
 Umoja wa Mataifa akiwemo Mratibu wa Mashirika hayo nchini Alvaro Rodriguez.
Kurejea
 kwa wingi kwa Wakimbizi hao ni pigo kisaikolojia kwa watu ambao 
walirejeshwa nyumbani kwa kuonekana kwamba hali ni shwari na walikuwa 
wameanza kuishi maisha ya kawaida.
Mkuu
 huyo wa kambi alisema idadi hiyo ikichanganyika na wengine imafanya  
kambi kuhemewa na kuonekana haja ya kutafuta eneo jingine la kupiga 
kambi kwa ajili ya Wakimbizi hao ambao mpaka mwishoni mwa wiki iliyopita
 walikuwa zaidi ya elfu 51.
“
 Kwa sababu tunapokea idadi kubwa ya waomba hifadhi toka Burundi, 
tumekuwa tukiongeza idadi ya vituo vya mapokezi ili kukidhi mahitaji ya 
kuwapokea  wakati tukisubiri maelekezo toka ngazi za juu za kuwahamishia
 Migunga Hills eneo linalopendekezwa kufunguliwa kambi ya Nyarugusu B” 
alisema Christopher mbele ya Waziri Chikawe.
Alisema
 walianza kupokea waomba hifadhi hapo kambini kuanzia Aprili 29, 2015 
kwa idadi ndogo kabisa ya watu 36, lakini idadi hiyo ilianza kuongezeka 
siku hadi siku na kufikia Mei 27 mwaka huu idadi yao ilifikia 48,333, 
idadi kubwa ikiwa wanawake na watoto.
Wakimbizi hao walikuwa wakipitia vituo vya Kigoma (27,638), Manyovu (4,439), Kilelema (1,603) na Kigadye (1,291).
Kambi
 hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 50,000 imeelemewa kwa sababu ya ujio 
mpya uliosababisha kuwepo kwa Wakimbizi zaidi ya 106,410.
Kuna
 matatizo zaidi ya milipuko ya wagonjwa kambi hii imechanganywa na  
Wakimbizi wa Kongo watu ambao hawana utamaduni wa pamoja na kuonekana 
hatari ya kukabiliana kwa kutosikilizana.
 Aidha kambi hiyo pamoja na kuwahifadhi waburundi wapo pia Wakimbizi kutoka Kongo wapatao 54,706; Burundi,3261 ; Rwanda 72; Uganda 17; Sudan Kusini wanane; Kenya 7; Somalia 3; Ethiopia 1; Zimbabwe 1; na Ivory coast 1.

Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke
 (wa pili kushoto) akizungumza jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya 
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),  Alvaro 
Rodriguez (kushoto) huku Mkuu wa kambi mpya inayotarajiwa kuanzishwa ya 
Nyarugusu B, Fredrick Nisajile
 (wa nne kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
 Mathias Chikawe (wa tatu kushoto) mara tu baada ya kuwasili na kusomewa
 taarifa kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani 
Kigoma. Wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama wa 
wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Akijibu 
 maswali ya waandishi wa habari walioambatana naye katika ziara hiyo 
kuhusu hali ya baadae ya Wakimbizi wa Kongo ambao wapo nchini kwa 
takribani miaka 19 sasa, Waziri Chikawe alisema kwamba serikali haina 
mpango wa kuwapa uraia kwa sasa ingawa Marekani imesema itawachukua 
Wakimbizi elfu 30 kuwapeleka kwao na kwingine duniani.
“hatuna
 mpango wa kuwapa uraia kwa sasa…” alisema Chikawe na kusema kwamba kwa 
kuondolewa kwa hao  wengine kutasaidia kupunguza idadi yao katika kambi 
hiyo.
Alisema kwamba ni lengo la serikali kuhakikisha kwamba kambi hiyo inapunguzwa ili kuweza kuchangia ipasavyo kwa hali bora ya Wakimbizi na kwamba mchakato wa kuwaangalia waomba hifadhi kama wanafaa kuwa Wakimbizi unaendelea.
Akizungumzia
 malalamiko ya upatikanaji wa chakula, Waziri Chikawe alisema kwamba si 
kweli kuwa kuna watu hawajapata chakula kwa siku saba la sivyo 
wangelikufa.
Alisema
 wengi wa Wakimbizi ni watoto na kwamba wanapoingia nchini wanapewa 
vyakula vikavu (kama biskuti)  lakini wakishafika kambini wanapewa 
chakula kilichopikwa na resheni ya siku 14 .
Alisisitiza kuwa kama kungelikuwa hakuna chakula watoto hao wasingeishi, labda kama wanataka kuongezewa chakula zaidi. (dk)
Kuhusu
 ujenzi wa kambi mpya Migunga alisema kwamba wataalamu wanaangalia 
barabara mbadala kwani iliyopo sasa pamoja na kuhitajika milioni 300 
kuitengeneza lakini bado kila mvua itakapokuwa inanyesha itahitaji 
kutengenezwa.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR),
 Joyce Mends-Cole katika mahojiano na waandishi wa habari aliishukuru 
serikali ya Tanzania kwa kufungua mipaka ili Wakimbizi waweze kuingia na
 kutoa eneo kwa ajili ya kambi mpya kutokana na ya sasa kujaa sana.
Aidha
 aliishukuru serikali ya Uingereza kwa kuwa ya kwanza kutoa misaada kwa 
ajili ya Wakimbizi hao na kutarajia nchi nyingine kama Marekani itafanya
 hivyo mapema ili kuisaidia serikali ya Tanzania katika kuhudumia waomba hifadhi.
Naye
 Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez 
amesema wanafanya kila linalowezekana ili kupunguza idadi ya Wakimbizi 
katika kambi ya Nyarugusu kwa kuwapatia eneo jingine la kujihifadhi.
Alisema
 kwa kuwatoa hapo watasaidia shule zilizofungwa ambazo zinasomesha 
watoto kutoka kwa Wakimbizi wa Kongo kurejea madarasani kukamilisha 
mtaala wao.

Mkuu wa kambi mpya inayotarajiwa kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile akifafanua jambo
 kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe wakati 
akitembelea na kukagua maeneo mbalimbali ya Kambi ya Nyarugusu iliyopo 
wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.

Waziri
 wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa 
Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la 
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa 
Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce 
Mends-Cole wakikagua sehemu wanayolala Waomba hifadhi wanaoendelea 
kuwasili katika kambi ya Nyarugusu ambayo inaelemewa kutokana na wingi 
wa Waomba hifadhi hao wanaoendelea kumiminika mjini Kigoma.

Muonekano wa moja ya chumba cha kulala familia
 za waomba hifadhi katika kambi ya Nyarugusu ambapo kifika muda wa 
kulala wanatandika mkeka chini katika vumbi hilo jekundu na kupata 
usingizi.

Waziri
 wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (mwenye suti ya kijivu),
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
 la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) pamoja na 
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR),
 Joyce Mends-Cole (kushoto) wakisikiliza hoja mbalimbali kutoka kwa 
Waomba hifadhi wanaohifadhiwa kwenye kambi ya Wakimbizi Nyarugusu 
iliyopo  wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma walipotembelea kambi hiyo 
kukagua kambi hiyo na kuangalia changamoto mbalimbali zinazowakabili na 
namna ya kuzitatua.

Waziri
 wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (mwenye suti ya kijivu) 
akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na 
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati 
walipotembelea kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo wilaya ya Kasulu 
mkoani Kigoma mwishoni mwa juma lililopita.

Waziri
 wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akigawa vifaa vya 
matumizi ya nyumbani ambavyo ni Blangeti, Mkeka, Kontena la kuhifadhi 
chakula na dumu la maji la lita 10 kwa mmoja wa Waomba hifadhi 
waliowasili siku ya ziara ya kutembelea kambi ya Nyarugusu mwishoni mwa 
juma wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mratibu 
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (mwenye shati jeupe).Kulia ni Mkuu wa
 kambi mpya inayotarajiwa kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile.

Waomba hifadhi  na familia zoa wakiwa katika foleni ya kupokea vifaa hivyo.

Waziri
 wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza na Waomba 
hifadhi katika kambi ya Nyarugusu wakati alipofanya ziara ya kutembelea 
eneo hilo akiwa ameambatana na Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa 
pamoja na Mwakilishi wa shirika la kuhudumia Wakimbizi nchini (UNHCR).

Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu
 akizungumza na mmoja wa wakinamama anayeishi kwenye kambi ya Wakimbizi 
Nyarugusu wakati wa ziara maalum ya kutembelea maeneo hayo iliyohusisha 
Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa.

 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
 la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez  na Mtaalam wa Mahusiano na 
Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu 
wakibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Kimataifa 
Ia Uhamiaji (I.O.M) (katikati) ambaye jina lake halikuweza kupatikana 
kiurahisi katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu
 mkoani Kigoma.

Mkurugenzi
 wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, 
Harrison Mseke (mwenye suti ya kijivu) akifafanua jambo kwa Mh. Mathias 
Chikawe alipotembela katika chumba maalum kichotumika kufanya usajili 
kwa Waomba hifadhi na familia zao kwa ajili ya kupewa hati ya kuwa 
Wakimbizi kamili kama watatimiza vigezo vinavyohitajika. Aliyeketi kulia
 ni Msajili wa Waomba hifadhi, Ndalo Charles Bogohe.

Zoezi la usajili likiendelea kwa familia za waomba hifadhi katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Wakinamama wakiandaa chakula cha mchana kwa familia zao kama walivyokutwa na kamera ya modewjiblog. 

Sehemu
 ya familia za Waomba hifadhi katika kambi ya Wakimbizi Nyarugusu, 
wilayani Kasulu, mkoani Geita wakiendelea kujipanga baada ya kuwasili 
kwenye eneo hilo.

Moja ya familia za waomba hifadhi ikiwa imejipumzisha mara baada ya chakula cha mchana huku nyuso zao zikionekana kuwa na furaha na matumaini mapya.

Hili ni eneo ambalo Waomba hifadhi  kutoka nchini Burundi wa kambi ya Nyarugusu wakiteka maji safi kwa matumizi yao.

Mkurugenzi
 wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, 
Harrison Mseke (kushoto) akizungumza jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika
 ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), 
 Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) wakati wakielekea kukagua vyumba vya
 madarasa katika shule ya msingi Mapendo ambayo yamegeuzwa kuwa nyumba 
za kulala Waomba hifadhi, kutokana na uhaba wa makazi ya kuishi kwenye 
maeneo ya kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wengine 
pichani ni baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama wa wilaya ya Kasulu 
mkoani Kigoma katika msafara huo.

Baadhi
 ya Waomba hifadhi katika kambi ya Wakimbizi Nyarugusu wakiwa 
wamempumzika huku wengine wakipata chakula cha mchana kama walivyokutwa 
na kamera ya modewjiblog.

Kinababa nao hushiriki kuandaa chakula cha mchana kwa familia zao kama huyu aliyekutwa na kamera ya modewjiblog.


Eneo
 la shule ya msingi Mapendo katika kambi ya Wakimbizi Nyarugusu ambalo 
kwa sasa linatumika kuhifadhi Waomba hifadhi wanaoendelea kuwasili 
nchini wakitokea Burundi kupitia mji wa Kigoma.

Madawati
 ya wanafunzi katika shule ya msingi Mapendo yakiwa nje ya madarasa 
yakitumika kuanikiwa nguo na huku wakati wa msimu wa mvua yakinyeshewa.

Waziri
 wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa 
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo 
(UNDP), Alvaro Rodriguez wakibadilishana mawazo na wasimizi wa kambi 
hizo za Nyarugusu wakati wa ziara ya siku moja wilayani Kasulu, mkoani 
Kigoma.

Mratibu
 Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) akiwa ameambatana na Waziri
 wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe wakikagua eneo jipya 
litakaloitwa Nyarugusu B lililotolewa na serikali kwa ajili ya Waomba 
hifadhi wanaoendelea kumiminika mjini Kigoma ambalo liko mbioni 
kutengenezwa na kukamilika ndani ya miezi 3 ijayo.

Eneo
 jipya la kambi ya Nyarugusu B ambalo limetengwa na serikali ya Jamhuri 
ya Tanzania kwa ajili ya makazi ya Waomba hifadhi wanataotenganishwa 
Burundi na Congo mara tu baada ya kukamilika.

Muonekano
 wa eneo jingine la makazi ya Waombahifadhi ndani ya kambi ya Wakimbizi 
Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.


Amani
 na upendo itawale kati yetu……ndivyo wanavyosema kwa pamoja baadhi ya 
watoto waomba hifadhi wakifurahia picha pamoja na Mratibu Mkazi wa 
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo 
(UNDP), Alvaro Rodriguez.
No comments:
Post a Comment