Burundi: waandamanaji wakata tamaa baada ya mkutano wa Dar es Salaam
Mtoto huyo anaangalia jinsi askari polisi wakiondoa vizuizi viliyowekwa kwenye barabara za mji wa Bujumbura, Mei 30 mwaka 2015.
Na RFI
Baada ya
mkutano wa marais wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki uliyofanyika
Jumapili Mei 31 jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania, raia katika
wilaya za mji wa Bujumbura, nchini Burundi, hasa waandamanaji wamekata
tamaa kufauatia uamzi wa marais hao.
Suala
muhimu la awamu ya tatu ya Rais Pierre Nkurunziza halikuchukuliwa uamzi
katika mkutano huo au hata kujadiliwa na marais hao wa nchi za Afrika
Mashariki. Watu wamechukizwa na jambo hilo na wako tayari kuendelea na
maandamano.
Katika
wilaya za mji wa Bujumbura kunakofanyika maandamano kama Cibitoke na
Nyakabiga, raia wamekata tamaa. Lakini pia wamekua na hasira, baada ya
mapendekezo yaliyotolewa katika mkutano wa jumuiya ya nchi za Afrika
Mashariki.(P.T)
Wakaazi
wa wilaya hizo walikua na matumaini kuwa viongozi hao kutoka nchi za
jumuiya ya Afrika Mashariki wangemtaka rais Pierre Nkurunziza kuacha
kuwania awamu ya tatu. Suala la kuahirishwa kwa uchaguzi kwa mwezi mmoja
na nusu halina mabadiliko yoyote katika msimamo wao.
"
Tumekataa tamaa moja kwa moja, kwa sababu hawakusema chochote kuhusu
awamu hii ya tatu ya rais Nkurunziza. Marais wa kanda hii hawana uwezo
wa kumshawishi Nkurunziza kuacha kuwania awamu ya tatu. Tunahitaji
jumuiya ya kimataifa kutusaidia ili tuweze kukabiliana na mgogoro huu ",
amesema raia mmoja aliyehojiwa na RFI.
" Hatukua
na matumaini makubwa kuhusu mkutano huo. Tuna machungu kutokana na
uamzi huo. huo ni usaliti wa moja kwa moja. Tutaendelea kuandamana,
tutaendelea na harakati zetu. Lakini ukweli hatimaye utashinda ",
wamesema raia wangine wa mji wa Bujumbura.
Serikali
ya Burundi imekaribisha mapendekezo ya marais wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki kuahirisha Uchaguzi kwa angalau mwezi mmoja na nusu ili
kukabiliana na hali ya kisiasa nchini humo.
Hata
hivyo upinzani unasema umesikitishwa na mapendekezo ya marais hao
waliokutana mwishoni mwa juma lililopita jijini Dar es salaam na wameapa
kuendelea na maandamano makubwa jijini Bujumbura leo Jumatatu.
Pacifique
Nininahazwe kiongozi wa maandamano amesema kuwa wamesikitishwa kuwa
viongozi hao wameshindwa kumwambia rais Nkurunziza kutowania urais kwa
muhula wa tatu.
Uchaguzi wa wabunge nchini Burundi umepangwa kufanyika tarehe tano mwezi huu, huku ule wa urais ukifanyika tarehe 26.
Itafahamika
kwamba rais wa Burundi Pierre Nkurunziza hakushiriki mkutano huo na
aliwakilishwa na waziri wake wa mambo ya nje Alain Nyamitwe. Hata rais
wa Rwanda Paul Kagame alisusia mkutano huo, akibaini kwamba viongozi wa
jumuiya ya Afrika Mashariki wamekua wakipigana chenga kuhusu uamzi mabo
unapaswa kuchukuliwa dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza.
No comments:
Post a Comment