Rais Obama akerwa na mauaji Marekani

Rais 
Barak Obama amesema mauaji ya watu tisa ndani ya Kanisa la Waafrika 
Wamarekani katika eneo la Charleston katika jimbo la Carolina Kusini 
yanaibua maswali kuhusu sehemu mbaya ya historia ya Marekani.
Katika 
hotuba yake iliyoonyeshwa katika televisheni muda mfupi baada ya polisi 
kumkamata mtuhumiwa ambaye ni kijana wa kizungu-- Bwana Obama amesema 
chuki miongoni mwa jamii kwa misingi ya rangi na imani ni kitisho kwa 
demokrasia ya Marekani na misingi yake.
Amesema 
mauaji ya watu wengi hayatokei kwa kiasi hiki katika nchi nyingine 
zilizoendelea, na ametaka kufanyika kwa mabadiliko ya pamoja katika 
fikra za Wamarekani kuhusu ghasia zinazosababishwa na matumizi ya 
silaha.(BBC)
No comments:
Post a Comment