Kuna mgomo wa kuuza mafuta Tanzania? Mbunge John Mnyika kairudisha hii tena Bungeni.
Kwenye Kikao cha Bunge jana JUNE 29 2015 Naibu Spika Job Ndugai alimwomba Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage atoe ufafanuzi kuhusu ujumbe uliosambazwa kwa message na Mitandaoni kwamba kuna mgomo wa kuuza mafuta ya petroli na dizeli.
Naibu Waziri akajibu kwamba ni uvumi usio na ukweli wowote, leo Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akawasha kipaza sauti na kuirudisha hiyo ishu tena >>>”Nimesimama
kutoa hoja kwamba shughuli za Bunge ziweze kusitishwa ili tuweze kwa
ajili ya kujadili hoja ya dharura ambayo ina athari kwa nchi na lina
maslahi kwa umma.
Jana
Naibu Waziri wa Nishati na Madini juu ya tetesi za mgomo wa mafuta
katika majibu yake alihakikisha kwamba hakuna mgomo, niliyasikiliza
majibu ya Waziri nikiwa Dar es Salaam.
Nilipotoka
Dar kuja Dodoma, kuanzia natoka Ubungo nimefanikiwa kupata mafuta mbele
kidogo ya Kibaha… Ukweli ni kwamba kulikuwa na mgomo, vituo vyote
nilivyosimama wanasema hawana mafuta>>>- John Mnyika.
Viko
vituo vilivyogoma kuuza na viko vichache sana vinavyouza vimeamua
kupandisha bei, naomba shughuli za Bunge zisitishwe na tujadili jambo
hili>>>- Mbunge John Mnyika.
Akapewa nafasi Naibu Waziri wa Nishati na Madini >>> “Tunayo
mafuta ya kutosha kati ya siku 12 mpaka siku 40, hatuna tatizo na kuna
meli ziko kwenye maji zinakuja… ninaihakikishia nchi hii kwamba haiwezi
kutokea tatizo.
Nawatuma
Wakaguzi Tanzania nzima muache tuwatafute, ukikutwa umekataa kuuza
mafuta faini ni milioni 20 na unaweza ukafungiwa kituo. Hii ndio kazi
niliyosomea muache watu waje kufaidi, ndio maana jana niliwaambia kichaa
karogwa tena… nilikuwa Mkaguzi sasa hivi ni Waziri muache nifanye kazi.
Watanzania
muwe na amani soko lina mafuta, huyo aliyetuma message atakamatwa na
tutampatia adhabu anayostahili, Bunge liendelee hii shughuli iko katika
mikono salama” >>>- Naibu Waziri Charles Mwijage.
Tukubaliane
kuna mambo ambayo yanawaumiza Watanzania kwa pamoja, tusikae
tukatengeneza jambo hili na siasa ndani yake… Maeneo mengine ukienda
unaangalia kwenye visima unakuta hamna mafuta. Kama tatizo ni la
kutengenezwa litakwisha, na kama lina namna nyingine yoyote Meli ziko
Baharini , zitakuja na litakwisha” >>>- Naibu Waziri wa Fedha, Adam Kigoma Malima.
Naibu Spika wa Bunge akafunga mjadala >>>
“Sioni sababu kulihusisha Bunge na jambo ambalo litakwisha kesho kwa
sababu bei ya leo na kesho itakuwa tofauti kwa sababu ya dola… Bila
EWURA kutangaza bei mpya hatuwezi kumaliza tatizo hili.
Kama hali itaendelea kuwa mbaya kesho na keshokutwa tutasema hili tulijadili, namini litaisha haraka sana” >>> — Job Ndugai.
No comments:
Post a Comment