Kiongozi wa ADF akabidhiwa Uganda

Kiongozi 
wa ADF akabidhiwa UgandaJeshi la Uganda linasema kuwa kiongozi wa kundi 
la waasi linalolaumiwa kwa mauaji ya karibu watu 1000 amekabidhibiwa 
Uganda baada ya kusafirishwa kutoka nchini Tanzania.
Jamil 
Mukulu ambaye alikamatwa nchini Tanzania mwezi Aprili, ni kiongozi wa 
kundi la ADF ambalo limelaumiwa kwa kuendesha mashambulizi mashariki mwa
 Uganda na mji mkuu Kampala.
Pia anatakikana kwa mashtaka yanayohusiana na vita nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Jeshi la Congo liliendesha oparesheni kubwa dhidi ya waasi wa ADF mwaka uliopita.CHANZO:BBC
IMECHOTWA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON
No comments:
Post a Comment