TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, July 17, 2015

Rais Kenyatta alivyokutana uso kwa uso na aliyeandika Barua kulalamika kwa Rais Obama

KENYATTA
Rais Uhuru Kenyatta na Babu Owino wamekutana uso kwa uso na kuingia kwenye headlines tena, tunajua kwamba ugeni wa Rais Obama ndani ya Kenya hauko mbali sana, ni kama wiki moja hivi imebaki.
sonu2
Rais Kenyatta na Babu Owino waliwahi kukutana kwa amani kabisa siku za nyuma.
Leo imeripotiwa na Citizen TV Kenya ikionesha Rais Kenyatta kuipuuzia barua ambayo iliandikwa na Kiongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi Chuo Kikuu Nairobi ambaye anaitwa Babu Owino ambayo aliandika na kutaka imfikie Obama.
Rais Kenyatta amekutana uso kwa uso na Babu Owino, akaanza kumuuliza imekuwaje akaandika barua ya kipuuzi kiasi kile? Rais Kenyatta akasema kama ni ishu ya Obama kutembelea Chuo atatembelea hata Chuo Kikuu cha Kenya na sio lazima aende Nairoibi University.
editor7956434643959646438-524x350
Babu Owino.
Nairobi ilimfahamu Babu Owino Jumatatu July 13 2015 baada ya barua yake kuingia mtaa ikiwa na Ujumbe mrefu kwa Balozi wa Marekani aliyeko Kenya kwamba kama Obama hatotembelea Chuoni kwao kuna wanafunzi 18 tayari wametishia kujiua !!
Babu Owino akaendelea kuandika kwamba kama Obama akipuuza mwaliko huo wa Chuo cha Nairobi, wanafunzi wa kike kama 31 watajipanga na kuukojolea mti ambao Obama aliupanda alipotembelea Kenya 2008 wakati akiwa Senator wa Jimbo la Illinois, Marekani.
Uhuru-Kenyatta

No comments:

Post a Comment