TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, July 17, 2015

Robinho kamfuata Asamoah Gyan China?

List ya mastaa wa soka waliotamba katika Ligi kubwa za soka duniani kucheza katika ligi kuu ya China imezidi kuongezeka baada ya staa wa Brazil Robson de Souza “Robinho” kujiunga na timu ya Guangzhou Evergrande inayochezea Ligi kuu China.
Robinho amesaini kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika na klabu ya Santos  ambayo alikuwa anaichezea kwa mkopo akitokea AC Milan ya Italia, Robinho amesaini mkataba wa miezi sita na klabu hiyo na anategemea kufanyiwa vipimo vya afya July 20… Robinho atakuwa anafundishwa na kocha wa zamani wa BrazilLuiz Felipe Scolari.

Robinho amewahi kutamba katika vilabu vya Manchester CityReal Madrid, Ac Milan na klabu yake ya Santos iliyomlea toka utotoni.
Hata hivyo Robinho anaingia katika list ya mastaa maarufu wa soka waliowahi kucheza soka China baada ya Asamoah Gyan kutoka Ghana kusaini hivi karibuni, Didier Drogba kutoka Ivory Coastna Nicolas Anelka kutoka Ufaransa

No comments:

Post a Comment