TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, July 28, 2015

Maneno ya James Mbatia alivyomkaribisha Edward Lowassa UKAWA

image 
Headlines baada ya headlines kuhusu siasa Tanzania zina uzito mpya kila siku… Imeandikwa sana Magazetini kuhusu Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa kuhama CCM, kilichoteka headlines July 27 2015 kimeongezea uzito kwenye ishu hiyo.
Viongozi wa Vyama vya UKAWA, Emmanuel Makaidi, Prof. Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia wamekutana Makao Makuu ya CUF Buguruni Dar na kutoa majibu kuhusu kumpokea Edward Lowassa.
Uchaguzi wa October 2015 ni fursa ya kipekee ya kuleta mabadiliko katika nchi yetu kuondoa ukandamizi uliojikita CCM… Watanzania wanahitaji Mabadiliko yenye fikra mpya na bunifu kwa maslahi ya Watanzania wote“>>> James Mbatia.
UKAWA tunahitaji Viongozi wenye sifa, uwezo na weledi katika kulinda, kuheshimu na kusimamia rasilimali za Taifa kwa maslahi ya Taifa.. Nachukua fursa hii kumualika Mheshimiwa Lowassa ajiunge na UKAWA na tuko tayari kushirikiana nae kuiondoa CCM madarakani” >>>> James Mbatia.
Bado Mbunge Edward Lowassa hajajibu chochote kuhusu kuendelea na CCM au kuhama

No comments:

Post a Comment