TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, July 22, 2015

BSS imeanza Dar, hizi ni pichaz ilivyokuwa Coco Beach. #July222015

Screen Shot 2015-07-22 at 7.50.38 PM 
Bongo Star Search imerudi tena mtu wa nguvu, huu ni msimu wa nane wa mashindano hayo tangu yameanza… mikoani kazi imeisha na washiriki wamepatikana, sasa ni zamu ya Dar es Salaam.
Baada ya Majaji kuwakusanya washiriki waliofanya vizuri Mikoa ya Mwanza, Arusha na Mbeya sasa kazi imeanza rasmi Dar es Salaam ambapo usaili ulianza July 22 2015 na utaendelea mpaka July 24, mchakato wote unaendelea pale Coco Beach.
Screen Shot 2015-07-22 at 7.50.52 PM
Meza ya Majaji, yuko Madam Rita, Producer Master Jay na Salama Jabir.
Kama kawaida majaji wa mashindano haya ni Madam Rita, Master J na Salama Jabir kazi yao kubwa ni kuwachuja wale wote wanaojitokeza kwenye usaili huu na hatimaye kuwapata wale bora zaidi watakaoiwakilisha Dar es salaam kwenye fainali msimu huu.
Screen Shot 2015-07-22 at 7.51.00 PM
Kazi ilikuwa kubwa kwa siku ya leo Coco Beach, watu wameonesha kupania kufanya kweli safari hii… walijitokeza kwa siku ya leo tu ni watu wengi sana na siku ikaisha kila kitu kikaenda vizuri.
Screen Shot 2015-07-22 at 7.51.10 PM
Chief Judge mwenyewe, Madam Rita.
Hapa chini nimekusogezea picha zikionyesha leo palivyokuwa Coco Beach.
Screen Shot 2015-07-22 at 7.51.27 PM
Mshiriki wa Bongo Star Search 2015 akijiandaa kuwaonesha Majaji kipaji 
Screen Shot 2015-07-22 at 7.51.38 PM
Foleni ya watu waliojitokeza kwenye usaili wa leo Coco Beach, hapa wakiwa wanachukua namba zao za kushiriki
Screen Shot 2015-07-22 at 7.51.47 PM
Foleni ya watu waliojitokeza leo Coco Beach, hapa wakisubiria kupewa namba zao za usahili.
Screen Shot 2015-07-22 at 7.52.03 PM
watu walikuwa wengi, foleni ndio kama unavyoona.
Screen Shot 2015-07-22 at 7.52.19 PM
Mshiriki mwingine aliyejitokeza siku ya leo, hapa akiwa anajiandaa kuonesha uwezo wake
Screen Shot 2015-07-22 at 7.52.33 PM
Watu na namba zao tayari, wakisubiri kuitwa

No comments:

Post a Comment