TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, July 30, 2015

Maelezo yaliyotolewa na Polisi Dodoma kuhusu Naibu spika Job Ndugai kumpiga mtu mpaka akazimia.

Ndugai 1 
Stori ilianza kusambaa kuanzia July 28 2015 kwamba Naibu spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai amempiga mtu mpaka akazimia na kisha baadae kufariki.
Hili tukio limefanya mpaka millardayo.com imtafute kamanda wa Polisi Dodoma Kamishna msaidizi mwandamiz wa Polisi David Misime ambaye ameyathibitisha haya >>> ‘Ukweli nilionao mimi ni kwamba tarehe 28 2015 jioni Joseph Elieza Chilongale alifika kwenye kituo cha Polisi Kongwa Dodoma akilalamika kuwa wakiwa kwenye mkutano wa kujinadi kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Ubunge jimbo la Kongwa kupitia CCM, alipigwa kwa kutumia fimbo kichwani na tumboni na Job Ndugai
Baada ya kutoa taarifa hiyo alipewa PF3 na akapelekwa Hospitali ambako amelazwa, tunachofanya ni kuendelea na uchunguzi kwa kupata maelezo kutoka kwenye eneo la tukio kutoka kwa watu waliokuwepo pale na baada ya kukamilisha upelelezi tutafikisha jalada kwa Mwanasheria wa serikali aelekeze hatua za kuchukua‘ – Kamanda Misime.
Kuhusu taarifa kwamba Joseph amefariki, Kamanda Misime amesemahizo taarifa sio za kweli sababu mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kongwa muda mfupi uliopita alikua pale Hospitali kuchukua maelezo yake kwa ajili ya kukamilisha upelelezi

No comments:

Post a Comment