Chelsea nao wametambulisha jezi zao watakazotumia msimu huu
Tukiwa tunasubiri kuanza kwa Ligi Kuu Uingereza
 msimu ujao vilabu kadhaa vimekuwa vikitangaza jezi za mechi za nyumbani
 na ugenini… Mara nyingi jezi zao huwa hazibadiliki rangi 
kinachobadilika ni muundo tu wa jezi na wakati mwingine nembo ya 
mdhamini kutegemeana na Mkataba ambao Klabu wanao.
Sababu mojwapo inayofanya vilabu vingi 
vikubwa duniani kubadili muundo wa jezi kila msimu, ni kusaidia klabu 
iweze kufanya biashara ya mauzo ya jezi kwani mashabiki wengi wa soka 
barani Ulaya huwa wanajivunia kuvaa na kumiliki jezi orijino ya klabu 
anayoipenda.
Shabiki wa klabu husika anaona fahari 
kuvaa jezi orijino na anajivunia pia, kuna vilabu ambavyo vimeshatangaza
 aina ya jezi watakazotumia msimu ujao ikiwemo Arsenal na sasa ni zamu ya Chelsea mtu wangu, nimekuwekea video ya jezi za Chelsea watakazotumia msimu ujao kwa mechi za  nyumbani.

No comments:
Post a Comment