Maoni ya viongozi wa Afrika kuhusu hotuba ya Obama
" Hakuna
mtu anapaswa kuwa rais wa milele ", amesema Rais Obama katika hotuba
yake kwa Umoja wa Afrika, akiwakemea viongozi wa Afrika wenye nia ya
kusalia madarakani wakati muda wao wa kuondoka madarakani unapofika
mwisho.
Na RFI
Rais wa
Marekani Barrack Obama ametamatisha ziara yake barani Afrika, kwa ujumbe
kwa viongozi wa bara hilo kuondoka madarakani muda wao unapofika
mwisho.
Akizungumza
katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa Jumanne wiki hii,
Obama amewaambia viongozi wa Afrika kuwa tabia ya kukataa kuondoka
madarakani inarudisha nyuma maendeleo ya demokrasia.
Ujumbe wa
Obama ulimlenga rais wa Burundi Piere Nkurunziza ambaye alikataa
kuondoka madarakani pamoja na viongozi wengine wanaobadilisha katiba ili
kuendelea kusalia madarakani.(P.T)
Lambert Mende, msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ametupilia mbali kauli za viongozi wa nchi za kigeni.
" Rais
Obama amerejelea maneno tunayosikia tangu miezi kadhaa kutoka kwa
viongozi kadhaa wa Magharibi ambao, wakati wanatembelea Afrika, hawawezi
kujizuia kutoa mafunzo kwa nchi za Afrika kama vile Afrika imekua nchi
moja, ikiwa na tatizo moja na ufumbuzi mmoja, kana kwamba Afrika imekua
na utaratibu wa Marekani kuhusu muda wa marais madarakani. Lakini sisi
katika DRC tunahisi kuwa jambo hilo halituhusu, ingawa tunaona kuwa ni
muhimu kuja na kutuambia jinsi ya kutatua matatizo yetu ya kitaasisi ...
", amesema Lambert Membe.
Waziri
mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, amekaribisha hotuba ya rais
Barack Obama juu ya haja ya kuimarisha demokrasia barani Afrika. Waziri
Mkuu wa Ethiopia, hata hivyo, alionekana akikosolewa na Barack Obama kwa
kuwanyanyasa na kuwazuia jela waandishi wa habari pamoja na kuwa
kandamiza wapinzani.
No comments:
Post a Comment