TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, July 30, 2015

Sababu ya Mbwana Samatta kugoma kujiunga na Zamalek ya Misri

Samatta 
Mbwana Samatta ni mshambuliaji wa kimataifa kutokea Tanzania anaeichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo alijiunga nayo mwaka 2011 akitokea Simba ya Tanzania na mpaka sasa amekua mmoja kati ya wachezaji mahiri wanaounda safu imara ya ushambuliaji kwa TP Mazembe na timu ya taifa ya Tanzania.
samata 
Samatta aliingia kwenye headlines siku kadhaa zilizopita baada ya kukataa kusajiliwa na klabu ya Zamalek ya Misri kwa euro milioni 1 kutoka TP Mazembe ambayo ni sawa na zaidi ya bilioni 2.3 za Kitanzania, kila media iliandika hii story nakuonekana kama Samatta amepoteza bahati.
Wakala wa mchezaji huyo Jamal Kasongo amezungumzia suala hilo na mpango wa Samatta licha ya kupewa ofa ya mshahara mkubwa.
Mbwana-2 
“La kwanza ni kweli maafisa wa Zamalek wawili walifika kipindi mimi nipo na Mbwana kipindi yupo katika mechi ya timu ya taifa kimsingi mimi niliweza kukaa nao chini kuweza kufanya nao majadiliano lakini lazima mchezaji ili ufikie malengo uweze kukaa katika mstari, msimamo wa Mbwana na msimamo wangu mimi kama mshauri wake ni Mbwana kuweza kucheza Ulaya”>>>Jamal Kasongo
MbwanaSamata-inaction120712BBP300 
“Wakatuma tena ofa wako tayari kumnunua TP Mazembe kwa euro milioni 1 na euro milioni 1 ni pesa nyingi na walikuwa tayari wakimuhitaji waweze kumpa mshahara ambao hakuna mchezaji ndani ya Afrika hii anaweza akalipwa lakini bado hili suala lilikuwa gumu kwani lengo kubwa ni Mbwana kucheza Ulaya”>>>Jamal Kasongo
Mbwana Samatta anamaliza mkataba wake na TP Mazembe mwezi April 2016 hivyo anaweza kuwa mchezaji huru na kuchagua timu ipi ya kwenda

No comments:

Post a Comment