Wanajeshi wanamaji wanne wauawa Marekani
Rais wa Marekani Barack Obama
Mtu
mwenye silaha amewaua askari wanne wa jeshi la wanamajiwa Marekani
katika shambulio lililofanywa kwenye majengo mawili ya jeshi hilo katika
mji wa Chattanooga, Tennessee. Wanajeshi hao wote waliuawa katika jengo
moja. Maafisa nchini humo wameyaita mauaji hayo kuwa ni Shambulio la
ndani. Shirika la Upelelezi la Marekani FBI linalochunguza mauaji hayo,
limesema halijajua bado kilichosababisha shambulio hilo.
Kufuatia tukio hilo maeneo kadhaa yamefungwa zikiwamo hospitali na shule ili kuchukua tahadhari.BBC
"Ni
mazingira ya kusikitisha kwa watu ambao wametumikia taifa kwa moyo
wote,kuuawa katika mfumo huu inasikitisha. Wakati maandalizi ya
mawasiliano na familia za wanajeshi hawa yakifanyika, naomba wafahamu
kuwa nazungumza kwa niaba ya raia wote wa Marakani kuelezea masikitiko
yangu na kuwahakikishia kuwa tupo nao katika mazingira haya magumu".
Naye Meya
wa jiji la Chattanooga Andy Berke alisema muuaji aliuawa na polisi. Pia
ofisa wa polisi pamoja na watu wengine wamejeruhiwa.
"tunafahamu
kuwa kuna watu wanne waliouawa. Tunafahamu kuwa muuaji pia aliuawa
katika eneo la tukio na pia afisa wa polisi mmoja wa Chattanooga
amepigwa risasi kwenye kifundo cha mguu na anatibiwa vilevile pale
Arlanga, pia kulikuwa na watu wengine waliopigwa risasi na wametibiwa
Mwanasheria mkuu wa jimbo la Tennessee, Bill Kilden, ameyaelezea mauaji hayo kama ugaidi wa ndani
No comments:
Post a Comment