Jamaa aliachiwa mtoto mchanga akaamua kumnywesha maziwa aliyochanganya na pombe
Dunia ina vituko vyake mtu wangu, na kwa wenzetu wa Marekani wakati mwengine vituko huzua madhara makubwa.
Nimekutana na hii moja inayomhusu Dontavian Eagle McCree mwenye miaka 19 aliyeachiwa jukumu la kukaa na mtoto wa dada yake wakati yeye akiwa kazini.
Siku moja wakati akiwa nyumbani na mtoto wa dada yake, Dontavian aliamua kumpatia mtoto huyo wa miezi 10 pombe, akachanganya pombe kwenye maziwa ya mtoto na kumnywesha.
Siku chache baadae mtoto alianza kuumwa 
na baada ya mama yake kugundua aliamua kumpeleka mtoto hospitali na 
ndipo alipogundua kuwa mtoto alinyweshwa pombe.
Dontavian
 amekamatwa na kupelekwa kituo cha polisi na thamani ya dhamana yake ni 
dola 15,000 ambayo ni sawa na Mil.30 za Kitanzania. Hali ya mtoto sio 
nzuri kabisa.



No comments:
Post a Comment