CHAMA CHA MADEREVA TANZANIA CHATOA TAMKO
Kaimu
Katibu Mkuu wa Chama Cha Madereva, Rashid Saleh (kushoto) akitoa tamko
hilo. Kulia ni mtunza hazina wa Chama hicho, Ramadhan Seleman.
....akihojiwa na waandishi wa habari.
CHAMA cha
Madereva Tanzania, kimetoa tamko rasmi juu ya marekebisho ya mikataba
yao, huku kikilalamikia kile kilichoitwa... “ukiukwaji wa makubaliano”.(P.T)
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar mapema leo, Kaimu Katibu Mkuu ambaye
pia ni msemaji wa chama hicho, Rashid Saleh alisema miongoni mwa mambo
na makubaliano ambayo anadai yamekiukwa ni pamoja na ucheleweshwaji wa
posho, ambazo kwa mujibu wa mkataba zilitakiwa kuanza kutolewa Julai
mosi mwaka huu, jambo ambalo halijatekelezwa.
Alisema,
kwa sasa wanafanya taratibu zote muhimu kwa lengo la kujua hatma yao
huku madeva wakitishia kugoma tena endapo haki juu ya mkataba huo
hazitafuatwa kulingana na makubaliano.
Hata
hivyo, msemaji huyo alilalamikia uzembe Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana
pamoja na Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) wa
kushindwa kusimamia waliyoiita “tume ya uchunguzi” ambayo imeonekana
kuchelewa kutimiza jukumu hilo.
No comments:
Post a Comment