Akon kuleta umeme Afrika
Muimbaji
wa miondoko ya R&b anayeongoza katika chati za juu za muziki huo
duniani 'Akon' ameamua kutumia tasnia yake ya muziki kukabiliana na
maendeleo endelevu ya watu wa barani Afrika.
Nyota
huyo wa R & B anazindua mpango maalumu wa mafunzo unaoitwa "Akon
Angaza Afrika" ambao una lengo la kutumia nguvu ya jua kuzalisha umeme
huku akiwa na matumaini ya kuwafikia watu milioni 600 barani wa Afrika.
Ufunguzi
wa huo umefanyika mjini mkuu wa Bamako nchini Mali, baadaye mafunzo hayo
yatafundisha kwa wadau wa mradi huo jinsi ya kutunza mifumo ya nishati
hiyo inayoendeshwa kwa nguvu ya jua.
Samba
Bathily ambaye ni mwanzilishi msaidizi wa mradi huo, anasema jua na
teknolojia hiyo ya ubunifu itasaidia kuleta umeme katika nyumba na
kwenye jamii kwa ujumla.
Kwa sasa anasema kuwa wanaimarisha utaalamu wa Kiafrika na kwamba hilo ni lengo lao.
Ameelezea
sababu ya kuwekeza zaidi kwenye nishatiya umeme kwamba ni moja ya njia
ya kutoa fursa za kiuchumi na huduma za kijamii kwa bara la Afrika
ambalo sehemu kubwa ni giza kutokana na ukosefu wa Nishati.
No comments:
Post a Comment