TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, July 12, 2015

STARS KUWEKA KAMBI UTURUKI KUJIANDAA NA MECHI DHIDI YA NIGERIA 

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inaweza kwenda kuweka kambi Uturuki mwezi ujao kujiandaa na mchezo wa pili wa Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 nchini Gabon dhidi ya Nigeria.
Na Stars inatarajiwa kwenda Uturuki baada ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza wiki ijayo Dar es Salaam.
Taifa Stars ilianza vibaya kampeni za Gabon 2017, baada ya kufungwa mabao 3-0 na wenyeji Misri mjini Alexandria katikati ya mwezi uliopita na sasa inaelekeza nguvu zake kusaka pointi tatu za kwanza katika mchezo wa kwanza Septemba.
Aliyekuwa kocha wa Taifa Stars tangu Aprili mwaka jana, Mholanzi Mart Nooij alifukuzwa kazi mwishoni mwa mwezi uliopita kutokana na matokeo mabaya, ikiwemo kufungwa mechi tano mfululizo na nafasi yake sasa anakaimu kocha mzalendo, Charles Boniface Mkwasa.(VICTOR)

Stars ambayo iliweka kambi ya wiki moja Addis Ababa, Ethiopia kabla ya kucheza na Misri Juni 14, itashuka dimbani tena Jumamosi ya Septemba 5, kumenyana na Nigeria mjini Dar es Salaam kabla ya kukamilisha mechi zake za mzunguko wa kwanza za Kundi G kwa kumenyana na Chad Machi 25 mwakani.
Malinzi ana kiu kubwa ya kuirejesha Tanzania kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika, ambazo mara ya kwanza na ya mwisho ilicheza mwaka 1980- na ndiyo maana amekuwa akihakikisha maandalizi yanakuwa mazuri.
MATOKEO NA RATIBA YA MECHI ZA KUNDI G
Jumamosi Juni 13, 2015
Nigeria 2-0 Chad
Jumamosi Juni 14, 2015
Misri 3-0 Tanzania
Jumamosi Sept 5, 2015
Tanzania v Nigeria
Chad v Misri
Ijumaa Machi 25, 2016
Chad v Tanzania
Nigeria v Misri
Jumatatu Machi 28, 2016
Tanzania v Chad
Misri v Nigeria
Jumamosi Juni 4, 2016
Chad v Nigeria
Tanzania v Misri
Jumamosi Sept 3, 2016
Nigeria v Tanzania
Misri v Chad

No comments:

Post a Comment