Haya ndio maamuzi ambayo Rafael Van der Vaart anajutia kwenye maisha yake ya soka
Kiungo wa kimataifa wa kiholanzi Rafael van der vaart ambaye amewahi kuitumikia Tottenham Hotspurs  kuanzia 2010-2012 akitokea katika klabu ya Real Madrid ya Hispania uhamisho ulioshangaza wengi kwa kiungo huyo kujiunga White Hart Lane.
Van der Vaart alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Spurs na
 alifanikiwa kuifungia magoli 28 katika mechi 78 na kuisaidia timu 
kufika hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya chini ya kocha Harry Redknapp wakati huo kabla ya kufukuzwa na nafasi yake kuchukuliwa na kocha Villas Boas.
Baada ya kuhama Spurs 2012 alijiunga na Hamburger SV ya Ujerumani kabla ya 2015 kurudi Hispania kwa mara nyingine tena ila katika klabu ya Real Betis, hadi leo hii Van der Vaart anasikitikia maamuzi yake ya kuhama Tottenham Spurs.
“Yalikuwa 
maamuzi binafsi ila wakati alipokuja Villas Boas aliniambia mimi sio 
chaguo lake la kwanza, huwezi kuamini nilikuwa nimecheza misimu miwili 
pale… kitu ambacho kilikuwa kigeni kwangu, nikaona bora 
kuondoka”>>>Van derVaart
“Ulikuwa 
ni uamuzi wa kijinga katika maisha yangu ya soka kuhama Tottenham, 
kiukweli najutia nilikuwa na misimu miwili mizuri katika maisha yangu ya
 soka”>>>Van der Vaart




No comments:
Post a Comment