Hii ndio hukumu iliyotolewa kwa mashabiki waliomsukuma mtu mweusi nje ya treni Ufaransa..
Unawakumbuka wale mashabiki wa Chelsea waliomshusha shabiki mwenzao kwenye treni  ya Paris Metro kisa ana asili ya Afrika?
Mahakana ya Stratford imewapiga marufuku kuhudhuria mechi zote za soka kwa miaka mitano ndani ya Ufaransa.
Richard Barklie, kutoka Carrickfergus, Northern Ireland, Joshua Parsons pamoja na William Simpson wote kutoka Surrey wamepigwa marufuku kuhudhuria mechi baada ya mahakama kuridhika na adhabu hiyo.

Jaji Gareth Branston
 alisema kwamba chuki ya kibaguzi iliyooneshwa na mashabiki wa Chelsea 
katika treni hiyo ya Paris na kiliharibu sifa  soka ya Uingereza.
Ishu hiyo ilitokea wakati mashabiki wa 
Chelsea walipokuwa katika mji wa Ufaransa wakishabikia mechi ya klabu 
bingwa Ulaya kati ya Chelsea na Paris Saint Germain July 17 2015.

No comments:
Post a Comment