Watanzania waliopewa tuzo na malkia wa Uingereza ndio hawa wamerudi Tanzania
Stori ninayotaka kukusogezea sasa hivi
ni hii kuhusu vijana wawili kutokea Tanzania (Given Edward & Angel
Benedicto) ambao wiki iliyopita walikabidhiwa tuzo na malkia wa
Uingereza kutokana na kile walichokifanya kwa jitihada zao.
Vijana walioteuliwa kuwania tuzo hizo za
malkia wa Uingereza walikuwa 60 kati ya mamia ya washiriki na dhumuni
kubwa ni kuwapongeza kwa mchango wao mkubwa wa kimaendelea katika nchi
zao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo July 1, 2015 Given Edward ambaye alikabidhiwa tuzo na malkia wa Uingereza alisema..’Kuna
rafiki yangu mmoja aliona shughuli ninazofanya akaniambia kuwa kuna
tuzo zinatolewa na malkia na anaamini kuwa naweza kupata kutokana na
kushughulia ninayoifanya’
‘Walihitaji
interview ambazo niliwahi kufanya na waandishi mbalimbali wakazihitaji
kuhusu project zangu na wakataka na makampuni niliyowahi kufanya nayo
kazi baada ya hapo basi wakatutangaza’
Sasa
hivi itakuwa ni rahisi zaidi ninapoenda kuongea na mashiriki au
makampuni kwasababu ninalofanya linathaminiwa lakini pia hata kwa
vijana wenzangu sasa hivi itakuwa rahisi kwangu kufanya nao kazi
kutokana na kile ninachokifanya kwani nina mipango mikubwa zaidi ya
hapo lengo langu ni kafanya process nzima ya kusoma iwe rahisi zaidi na
wanafunzi wawe wanapenda zaidi kusoma kwasababu sasa hivi wanafunzi
wengi wanachukulia kusoma kama adhabu kuliko kama zawadi..’alisema
Wa pili ni Angel Benedicto ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani (House Girl)
alimaliza kidato cha nne akaona aweza kuendelea na masomo, hali ni
ngumu kwenye kimaisha akawa ni mfanyakazi wa ndani au msichana wa kazi
za ndani (House Girl) lakini leo hii ameweza kutumia nguvu yake ya
ushawishi ya kuongea na vijana na kazi yake imetambuliwa na malkia na
akapewa tuzo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo July 1, 2015 Angel Benedicto alisema…’Tuzo
hii inanisaidia kwamba niweze kuwafikia vijana zaidi ambao ni
wafanyakazi wa nyumbani hasa wa kike ambao wamekata tamaa tuweze
kuwasaidia kwamba haujazaliwa kuwa mfanyakazi wa nyumbani tu , kuna
nafasi nyingi pia kwa hiyo kama ni ujasiriamali jitahidi kama unapata
elfu 40 yako tunza…
No comments:
Post a Comment