Hata South Africa wana matatizo yao pia, mvulana apoteza maisha baada ya mchezo huu kwenda vibaya!
Loyiso kijana wa miaka 19 ameweka headlines kubwa sana jijini Johannesburg South Africa baada ya tukio la janga la treni kutokea mjini hapo.
Kijana huyo aliyekuwa kwenye kipindi cha
 mitihani alifariki siku ya jana baada ya kuthubutu kucheza mchezo wa 
kurukaruka ndani na nje ya treni iliyokuwa kwenye spidi kali, mchezo 
unao hatarisha maisha.
Loyiso
 alikuwa njiani kuelekea shule wakati mchezo huo ulipogeuka kuwa tukio 
la kutisha, baadhi ya abiria waliokuepo kwenye treni hiyo walisema…
>>> “alikuwa
 anarukaruka ndani na nje ya treni hii na kwa bahati mbaya aliteleza na 
kuingia katikati ya reli za treni tukiwa tunakaribia kituo cha Chiawelo 
Railway Station”.<<< 
>>> “walikuwa
 kikundi…kikundi cha vijana waliokuwa wanacheza mchezo huu, lakini kwa 
bahati mbaya huyo mmoja aliteleza na kuingia chini ya reli ya treni na 
kichwa chake kilisagwa. Ni tukio la kutisha sana na linavunja moyo.<<<
Vyombo vya kulinda usalama kwenye kituo cha Chiawelo Railway Station vimekuwa
 vikijaribu kupambana na tatizo la mchezo huu kwa muda mrefu sana kwani 
limekuwa tishio kwa jamii. Tukio hili limewaacha ndugu, jamaa, marafiki 
pamoja na wanafunzi wengi na masikitiko makubwa.



No comments:
Post a Comment