TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, July 24, 2015

Licha ya kufungwa 4-2 na New York Red Bulls Jose Mourinho hakaukiwi maneno

jose-46
Baada ya klabu ya Chelsea kupoteza mchezo wa kwanza wa International Champions Cup dhidi ya New York Red Bulls kwa goli 4-2, kocha wa timu hiyo Jose Mourinho hakaukiwi maneno mdomoni mwake kama alivyozoeleka !!
Mourinho ambaye anafahamika kwa tabia yake ya kupenda kuongea, kubeza na kujitamba amefurahisha wengi baada ya kuzungumza kauli nyingine za kujiamini  kabisa!!
Mourinho-Chelsea
“Walikuwa na hamasa na furaha ya kucheza dhidi yetu, walituonesha mchezo bora na tulijifunza”>>>Mourinho
“Tumefanya mazoezi mara 11 ndani ya siku sita, tunawaamini hawa wachezaji, tuliwahi kucheza mara 10 na hii timu tumeshinda mara 9 lakini kipindi cha pili kilikuwa majanga”>>>Mourinho
Chelsea's coach Jose Mourinho waits for the kick off of their Champions League Group G soccer match against Sporting Lisbon at the Estadio Jose Alvade in Lisbon, September 30, 2014.  REUTERS/Hugo Correia (PORTUGAL  - Tags: SPORT SOCCER HEADSHOT)
Mourinho kama ilivyo kawaida yake, hajaishiwa kingine cha kuongea >>>>“Mimi ni kocha wa timu bora Uingereza, tuna wachezaji wa viwango vya juu hivyo hakuna udhaifu”>> Mourinho
1411145295811_wps_10_Chelsea_FC_via_Press_Asso (1)
Mourinho ni kocha mwenye utamaduni wa kujisifia, kuna wakati aliwahi kumponda mchezaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kuhusu Cristiano Ronaldo, alisema yeye anamtambua Ronaldo mmoja tu naye ni Ronaldo de Lima na hakuna mwingine.

No comments:

Post a Comment