Hali si shwari ndani ya FIFA, kashfa zazidi kufichuliwa !!

Wapelelezi wanaofatilia kashfa ya rushwa
 inayohusu shirikisho la soka ulimwenguni FIFA wameahidi kufichua 
makubwa zaidi baada ya kugundua siri nzito zilizojificha kwenye mchakato
 wa kuchagua mwenyeji wa kombe la dunia.
Wapepelezi hao wakiongozwa na Mwanasheria mkuu wa Uswisi, Michael Lauber wamesema
 kuwa kuna matukio karibu 53 ya uchakachuzi na utakatishaji haramu wa 
fedha ambayo yamegundulika kwenye michakato tofauti ya kumpata mwenyeji 
wa michuano ya kombe la dunia na matukio haya yamehusishaa watu wazito 
ambao kama yatagundulika undani wake yatazua hofu na utata mkubwa.
Mwanasheria huyo ameonya kuwa hatajali 
kama upelelezi wake utasababisha hasara ya fedha  au kupokonywa uwenyeji
 kwa nchi za Urusi na Qatar na anachojali ni ufanisi wa kazi yake na si 
kitu kingine.
Imedaiwa kuwa upelelezi huu unahusisha kuhojiwa kwa viongozi wa juu wa FIFA akiwemo rais wa zamani Sepp Blatter ambaye hivi karibuni alitangaza kujiuzulu siku chache baada ya kuchaguliwa kwa kipindi cha tano.
Viongozi kadhaa wa zamani wa FIFA wakiwemo Mmarekani, Chuck Blazer na rais wa zamani wa chama cha soka cha Trinidad and Tobago, Jack Warner wameahidi kutoa ushirikiano kwa wapelelezi huku wakiahidi kuwa watazungumza bila kuficha.


No comments:
Post a Comment