Mbowe ahukumiwa mwaka mmoja
MAHAKAMA
ya wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, imemtia hatiani na kumhukumu
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kwenda jela mwaka mmoja au
kulipa faini ya Sh milioni moja, kutokana na kesi iliyokuwa ikimkabili
ya kumshambulia mwangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Akisoma
hukumu hiyo iliyohudhuriwa na wabunge wengi wa Chadema, Hakimu Mkazi
Mfawidhi, Denis Mpelembwa, alisema mahakama imemkuta Mbowe na hatia,
hivyo kutakiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini
kiasi cha Sh milioni moja.
Mbowe
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, katika kesi hiyo ya jinai namba 73
ya mwaka 2011, alidaiwa kumshambulia Nassir Yamin, katika Kijiji cha
Nshara, kata ya Machame Kaskazini, Wilaya ya Hai, katika uchaguzi mkuu
wa mwaka 2010. Mpelembwa alisema mahakamani hapo kuwa hukumu iliyotolewa
mahakamani hapo imezingatia ushahidi uliotolewa kwa upande wa
mlalamikaji Nassir Yamini. (DK)
Kwa
upande wake, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe akizungumza mahakamani hapo,
alisema hukumu iliyosomwa mahakamani hapo haijamtendea haki.
Alisema
kesi yake hiyo haikustahili kuchukua muda mrefu kama mahakama
ilivyofanya kwa kuchukua zaidi ya miaka mitano bila kusomewa hukumu.
Hata
hivyo, Mbowe amelipa kiasi cha fedha Sh milioni moja alichotakiwa kulipa
kama hukumu ilivyoeleza, kwa kumtaka kulipa kiasi hicho cha fedha au
kwenda jela mwaka mmoja.
Lema na Polisi
Wakati
Mbowe akihukumiwa, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema jana alishindwa
kuzuia hasira zake na kutaka kupigana na mmoja wa askari polisi katika
kituo cha kuandikisha wapigakura cha Mkombozi kata ya Sokoni One, Jimbo
la Arusha.
Tafrani
hii ilitokea baada ya kukuta polisi huyo akiandikisha wananchi
wanaohitaji vitambulisho, kabla ya kuingia ndani ya chumba cha
waandikishaji.
Vurugu
hizo zilitokea saa 5:30 asubuhi, mara baada ya Lema kuingia eneo hilo
akitembelea vituo vya kuandikisha wapiga kura kuangalia hali halisi.
Alipofika
kwenye kituo hicho alikuta mmoja wa Polisi akiwa amevaa kiraia (Jina
halikupatikana mara moja), akiwa na daftari dogo akiorodhesha majina ya
wapiga kura kwa lengo la kupunguza foleni.
Akizungumza
na wananchi huku Lema akiwa amezungukwa na askari polisi, alisema huo
sio utaratibu wa kufanywa na polisi na hata Tume hairuhusu Polisi
kufanya kazi hiyo bali kulinda amani tu.
Hata
hivyo, Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi cha Arusha, Thomas Maleko,
akimtuliza hasira Lema akisema wao wanafanya kazi hiyo, ili kuwapunguzia
adha wananchi ambao wanafika kituoni saa 9:00 usiku, hadi siku ya pili
wanakaa kutwa nzima bila kupata fursa ya kuingia chumba cha
kujiandikisha.
Alisema
kutokana na hali hiyo, ndipo Polisi walipoamua kuandikisha watu kwa
makubaliano na waandikishwaji wenyewe, ili waondoke nyumbani wakafanye
kazi zingine na kesho yake wakirejea wanapata fursa hiyo.
“Hawa
watu hata wakikaa hapa hawawezi kuingia ndani ya chumba husika, maana
kuna kompyuta moja tu, hivyo wanapigwa na jua, hivyo utaratibu huu sisi
tumeona ni mzuri, tunaandika jina la mtu kisha tunamruhusu aende
nyumbani hadi kesho aje anaingia ili kupata kitambulisho,” alisema.
Hata
hivyo, licha ya maelezo ya polisi, Lema hakukubaliana nayo na
kuwasiliana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Juma Idd ambaye alimtuma
Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi, ambaye naye hakutaka kuzungumza chochote na
waandishi wa habari na pia hakutaka kutaja jina lake. (HABARI LEO)
No comments:
Post a Comment