Maafisa wa Marekani kumchunguza Blatter
Sepp Blatter
Imeripotiwa
kuwa Raisi wa Fifa,Sepp Blatter anafanyiwa uchunguzi na maafisa wa
marekani ili kuthibitisha tuhuma za rushwa zinazomkabili vyombo vya
habari vya Marekani vimeripoti.
Taarifa hiyo inakuja baada ya Blatter kutangaza kuwa atajiuzulu wadhifa wake.
Wakati
ambao waendesha mashtaka nchini Marekani wanaoifuatilia tuhuma za rushwa
walikamata maafisa saba wa Fifa nchini Switzerland kati ya watu 14
wanaotuhumiwa kwenye kashfa hiyo.
Hata hivyo Blatter alisema anatumia mamlaka aliyopewa hata kama hayakubaliwi na kila mtu duniani.
Fifa inahitaji mabadiliko makubwa ili kukemea rushwa.
Mwandishi
wa BBC,Nick Bryant mjini New York anasema kuwa bado maafisa hao wa
marekani wana matumaini ya kupata ushirikiano kutoka kwenye takwimu za
Fifa kwa sasa ili kubaini namna ambavyo mzunguko wa pesa chafu
unavyomuhusisha Blatter.
Katika
taarifa iliyoripotiwa kutoka kwa maafisa wa Marekani wiki iliyopita
kuhusu rushwa katika shirikisho hilo la soka ulimwenguni, Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Loretta Lynch haikumshutumu Blatter moja kwa moja .
Ingawa alisema kuwa huu ni mwanzo tu wa uchunguzi na si mwisho.
Mwandishi wetu anasema huu ni msingi wa maafisa wa marekani katika kuikomboa dunia katika majanga makubwa kama haya.
Mwanzoni
FBI,mamlaka ya ndani ya huduma za Mapato nchini Marekani na mwanasheria
wa New York , ambaye alishiriki katika uchunguzi huo walisema kuwa
hawana maoni juu ya kujiuzulu kwa Blatter.CHANZO:BBC (Muro)
No comments:
Post a Comment