Newcastle imempa ulaji kocha wa zamani wa Uingereza
Newcastle
United imemtangaza Steven McClaren kuwa kocha mpya wa klabu hiyo baada
ya kumtimua kocha wake John Carver aliyenusurika kukishusha daraja
kikosi hicho cha St James Park.
McClaren
mwenye umri wa miaka 54 anachukua nafasi ya John Carver ambaye
alifukuzwa siku ya Jumapili iliyopita, kocha huyo wa zamani wa Uingereza
pia amewekwa katika bodi ya timu hiyo.
McClaren
amepewa kandarasi ya miaka mitatu ambayo huenda ikaongezwa na kufikia
miaka nane endapo ataisaidia klabu hiyo kutwaa taji lolote kwenye muda
huo wa miaka mitatu aliyopewa kwa sasa.
Kocha
huyo amesema; “nimeheshimiwa kuteuliwa kuwa kocha mkuu wa Newcastle
United FC. Hii ni klabu kubwa yenye urithi wa kipekee”.(P.T)
“Mashabiki
wake ni watulivu na wana moyo na timu yao, mbali na yote bado wamekuwa
ni waaminifu. Tutafanya kadri tuwezavyo tuwazawadie mafanikio”, amesema.
“Kuna
kazi kubwa ya kufanya, lakini klabu imeweka bayana kwamba inahitaji
mafanikio, na nisingekuja hapa kama ningekuwa siamini kama wapo makini.
Timu hii imekaa kwa muda mrefu bila kushinda taji lolote, na kushinda
taji ndio lengo langu la kwanza kabisa hapa”, ameongeza.
“Nimeshashinda
mataji nikiwa kama kocha, timu kama Newcastle United inatakiwa kushinda
vikombe na kumaliza msimu wa ligi kuu ikiwa kwenye nafasi nane za juu.
Nitawapa mashabiki wa Newcastle kitu ambacho watakuwa wakijivunia, na
kazi hiyo inaanza sasa”, alimaliza.
Kocha
huyo wa zamani wa Uingereza ambaye alipigwa kalamu na klabu ya Derby
County mwezi Mei, aliikataa kazi hiyo mara mbili baada ya Alan Perdew
kuondoka na kabla ya kukamilika kwa mechi tatu za mwisho za msimu huu.
No comments:
Post a Comment