WTO: India imekiuka sheria za biashara
India imezuia kuku wa Marekani kuingia nchini humo kwa hofu ya ugonjwa wa mafua ya ndege
Shirika
la kimataifa la biashara duniani, WTO limesema India haijafanya uamuzi
wa haki kuzuia uingizaji wa kuku na mayai kutoka Marekani kwa hofu ya
ugonjwa wa mafua ya ndege.
Shirika
hilo linaendelea kushikilia uamuzi uliotolewa katika mahakama ya
usuluhishi ya masuala ya kibiashara uliofanyika Oktoba mwaka jana. India
iliweka vikwazo vya kibiashara tangu mwaka 2007, ikisema inataka kuzuia
mafua ya ndege kuingia katika nchi yake. Ingawa WTO inasema sheria
zilizowekwa na India hazikufuata viwango vya kisayansi vya kimataifa.
Uongozi
wa serikali ya Rais Obama umekubaliana na uamuzi huo, ingawa kiwanda cha
kuku nchini Marekani kimeona kuwa India inaacha kupokea kuku wenye
thamani ya dola milioni mia tatu.CHANZO:BBC (Muro)
No comments:
Post a Comment