Baada ya ajali ya lori la mafuta Nigeria, hii nyingine ni kituo cha mafuta kuwaka moto Ghana
Mapema 
wiki hii Habari makini blog iliandika stori ya ajali ya lori la mafuta kuua 
zaidi ya watu 90 Nigeria ikiwa ni baada ya kuwa kwenye mwendo mkali na 
kugonga watu na magari yaliyokuwa kwenye kituo cha abiria.
Lakini 
leo Ghana nayo imeingia kwenye headlines baada ya kituo cha mafuta 
kulipuka na kuua watu wanaokadiriwa kuzidi 90 katika mji mkuu wa nchi 
hiyo Accra.
Mlipuko
 huo umetokea baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko katika maeneo 
mengi ya mji huo ambapo pia imewaacha watu wengi bila makazi huku sehemu
 kubwa ya mji ikiwa gizani kutokana na kukatika kwa umeme.
Idadi 
ya watu waliofariki huenda ikaongezeka kwani watu wengi wamepoteza 
maisha baada ya kuwepo kituoni hapo wakijikinga na mafuriko yaliyotokea 
na huenda idadi ikaongezeka kutokana na baadhi ya miili kuwa bado 
haijapatikana.



No comments:
Post a Comment