Nusu fainali za michuano ya French Open
Andy
Murray mcheza tenis wa Uingereza akitinga nusu fainali za michuano ya
French Open ya mwaka 2015Andy Murray amefanikiwa kumbwaga mpinzani wake
David Ferrer kwa mara ya kwanza katika uwanja wa udongo na kutinga kwa
mara ya tatu katika nusu fainali za French Open.
Mwingereza
huyo wa tatu kwa ubora duniani kwa wanaume alishinda 7-6 (7-4) 6-2 5-7
6-1 na atakabiliana na Novak Djokovic anayeongoza kwa ubora katika
mchezo huo wa tenisi kwa wanaume.
Ushindi huo unampeleka Murray katika hatua ya nusu fainali ya michuano mikubwa kwa mara ya 16.
Naye
Rafael Nadal amesema atapigana kuhakikisha anarejea katika ubingwa wa
michuano ya French Open baada ya kutolewa na Novak Djokovic katika hatua
ya robo fainali. Hii ni mara ya pili kwa Nadal kufungwa mjini Paris.
Djokovic
kutinga hatua ya nusu fainali amemshinda Nadal kwa seti 7-5 6-3 6-1 na
sasa ana kwa ana na Andy Murray katika nusu fainali.
Na kwa
upande wa kina dada, mchezaji nambari moja Serena Williams alihitaji
dakika 65 tu kumrarua mpinzani wake Sara Errani kwa seti 6-1 6-3 na
kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya French Open katika uwanja wa
Roland Garros. Sasa atapambana na Mswiss Timea Bacsinszky. Huku bingwa
mtetezi wa michuano hiyo kwa wanawake Maria Sharapova, ameng'olewa
katika michuano hiyo kwa kucharazwa na Lucie Safarova kutoka Czech kwa
seti 7-6 (7-3) 6-4.CHANZO:BBC (Muro)
No comments:
Post a Comment