Kashfa ya rushwa FIFA, mmoja amekiri kupokea, mwingine aapa kufichua ufisadi..!!
Wakati
sakata kuhusu tuhuma za rushwa likiendelea kuliandama Shirikisho la soka
duniani FIFA huku baadhi ya Maofisa wake wakishikiliwa na Rais Blatter
kujiuzulu, kuna habari nyingine inayohusiana na kashfa hiyo.
Taarifa iliyopokelewa na Wizara ya sheria ya Marekani inayoelezea jinsi afisa wa zamani wa FIFA Chuck Blazer
kukiri yeye na viongozi wenzake kupokea rushwa ili kuichagua Afrika
kusini kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la duniani mwaka 2010.
Mbali na Blazer pia aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo Jack Warner amesema kwamba atafichua kila anachojua kuhusu ufisadi ndani ya shirikisho hilo.
Taarifa
hiyo imeweka wazi mtandao wa malipo uliofanywa ndani ya Shirikisho hilo
wakati wa uchunguzi uliofanywa na wapelelezi wa Marakeni FBI
Kitendo
cha Afisa huyo wa zamani wa FIFA, Chuck Blazer kukiri kupokea rushwa
sasa huenda ikaibua mengi kwenye kashfa ya rushwa inayowahusu FIFA.
Mmarekani huyo kwenye taarifa hiyo
inadai alikuwa ni mmoja wa watu waliosuka mipango ya kupokea rushwa
katika tukio jingine la fainali la kombe la dunia 1998.
Marekani imefungua kesi ya rushwa
inayowakabili maafisa wa FIFA..kesi inayohusu kupokea rushwa ya dola
milioni 150 jambo lililofanya Rais wa FIFA Sepp Blatter kuamua kutangaza
kujiuzulu.
No comments:
Post a Comment