Mikoa ya Shinyanga na Mwanza yaendelea na ubabe mbio za baiskeli
Mshindi
wa mbio za Acacia Tufanikiwe Pamoja Lake Zone Cycle Challenge, Masunga
Duba aliyeinua mikono akishangilia mara baada ya kumaliza mbio hizo
akiwa mbele ya wenzake. Mshindi huyo anatoka mkoa wa Shinyanga.
Mmoja wa washiriki wa mbio hizo akinywa maji wakati wa mashindano hayo.
Washiriki wa mbio za Acacia tufanikiwe pamoja lake zone cycle challenge wakimenyana vikali wakati wa mashindano hayo. (DK)
Makamu
wa rais wa Kampuni ya Uchimbaji wa dhahabu ya Acacia, Deo Mwanyika (wa
kwanza kushoto) akifurahia jambo na Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni
ya Acacia, Mishel Ash, (wa pili kutoka kushoto) ambaye pia ni kaimu
Meneja Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu.
Washindi
wa mbio za wanawake (kilometa 80). Aliyesimama katikati ni Martha
antony ambaye ndio aliibuka mshindi wa kwanza, akifuatiwa na Laulensia
Luzuba, (mwenye mtoto) aliyekuwa mshindi wa pili na Veronica Saimon (wa
kwanza kushoto) aliyejinyakulia nafasi ya Tatu.
Afisa
mkuu wa uendeshaji wa kampuni ya Acacia Mishel Ash akimvisha medali
mshindi wa mbio hizo Martha Antony wakati wa Hafla ya Kutoa zawadi kwa
washindi.
Washiriki
wa mbio za baiskeli zijulikanazo kama “Acacia Tufanikiwe Pamoja Lake
Zone Cycle Challenge” kutoka mikoa ya Shinyanga na Mwanza wameendelea
kuudhihirisha umma wa wakazi wa kanda ya ziwa na watanzania kwa ujumla
kuwa mpaka sasa hawana mpinzani baada ya washiriki wa mbio hizo kuibuka
kidedea katika fainali za kumtafuta mshindi wa kanda hiyo.
Washiriki
wa mikoa hii miwili wamejinyakulia nafasi zote za juu na hivyo
kuwashinda wenzao wa mikoa mingine ya Kanda ya ziwa ikiwemo Kagera,
Mara, Geita na Simiyu.
Katika
mbio za wanaume za umbali wa kilometa 156.6 kutoka Kahama mpaka Tinde na
kisha Kurejea Kahama, mshindi wa mwaka jana Masunga Duba (Mwanza)
aliibuka tena kidedea huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Lupilya
Hamis(Shinyanga) na nafasi ya tatu ikimuendea Kulwa Tuki(Shinyanga),
washindi hawa wamejinyakulia kitita cha pesa taslimu Sh1,500.000/- kwa
mshindi wa kwanza, Sh1,200.000/= mshindi wa pili na Sh800,000/= kwa
mshindi wa tatu.
Kwa
upande wa mbio za wanawake za umbali wa kilometa 80, kutoka Kahama mpaka
Mwakata Kisha kurejea Kahama, timu ya mkoa wa Mwanza imedhihirisha kuwa
wao bado ni mabingwa kwa kuibuka tena washindi wa mbio hizo, huku
mshindi wa mbio za Mwaka jana Martha Antony, akiibuka mshindi wa kwanza
akifuatiwa na Laulensia Luziba na nafasi ya tatu ikienda kwa Veronica
Simon. Washindi hao wamepata zawadi ya pesa taslimu Sh1,200.000/= kwa
mshindi wa kwanza, Sh800,000/= mshindi wa pili na Sh600,000/= mshindi wa
tatu.
Mbio hizo
ambazo zimeandaliwa na Chama cha Baiskeli Tanzania (CHABATA) kwa
udhamini wa kampuni ya uchimbaji wa Madini ya Acacia, inayomiliki migodi
ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi, yote ikiwa mikoa ya kanda ya
ziwa, kupitia mpango wake wa Tufanikiwe Pamoja ikiwa ni mara ya pili
sasa ambapo mashindano ya mwaka huu yameonyesha mafanikio makubwa
kutokana na maandalizi mazuri yaliyofanyika.
Akizungumza
na washiriki wa mashindano hayo Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpyesa,
ambaye alikua mgeni rasmi wa fainali hizi, amesema ana imani kuwa
mashindano hayo yatasaidia kuibua vipaji ambavyo vitauletea sifa mkoa wa
Shinyanga, Kanda ya ziwa na hata taifa kwa ujumla kwani baiskeli kwa
maeneo hayo ndiyo jadi yao.
Awali
akimkaribisha Mkuu wa wilaya kuzungumza na washiriki hao, Makamu wa Rais
wa Acacia Deo Mwanyika amesema kampuni ya Acacia imekuwa ikifanya
shughuli za uchimbaji unaojali na ndio maana iliona vyema kuweka
udhamini wake pia katika mchezo wa baiskeli, “toka tuanze huu sasa ni
mwaka wa pili na tunayaona mafanikio makubwa kwani hata maeneo ambapo
mchezo huu ulikuwa hauchezwi sasa unachezwa, hali ambayo imeongeza
hamasa na idadi ya washiriki.”
Aidha
Makamu wa Rais huyo wa Acacia amesema mipango ya kampuni kwa sasa ni
kuona pia inashiriki katika kuendeleza michezo mingine ikiwemo na soka
No comments:
Post a Comment