Jack Warner alia Marekani inalipa kisasi
Aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho la Soka Duniani FIFA, Jack Warner
Aliyekuwa
makamu wa rais wa shirikisho la Soka Duniani FIFA, Jack Warner,
ameituhumu Marekani kwamba inafuatilia mashtaka ya rushwa dhidi ya
maafisa waandamizi wa shirika hilo kwa sababu imeshindwa kuwa mwenyeji
wa kombe la dunia la mwaka 2022.
Akiandika
katika gazeti ambalo analolimiliki huko Trinidad na Tobago, bwana
Warner amesema tuhuma hizo dhidi yake na wengine kumi na tatu
zinaonyesha kwamba Marekani inaegemea upande mmoja.
Warner
amekana tuhuma hizo. Shirikisho hilo la Soka Duniani limegubikwa na
tuhuma za rushwa kwa kipindi cha wiki mbili mfululizo. Akiandika katika
gazeti lake linaloitwa Sunshine, Warner anaelezea mashtaka ya Marekani
dhidi yake kuwa ni uonevu na yaliyoegemea upande mmoja.(P.T)
Warner
amesema Marekani ambayo inajifanya kuwa ni polisi wa dunia, imehamasika
kuchukua hatua hiyo baada ya kushindwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya
kombe la dunia ya mwaka 2022.Warner, mwenye umri wa miaka 72 amekana
tuhuma za kupokea rushwa ya dola milioni kumi za kimarekani kutoka
Afrika Kusini baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la
dunia ya mwaka 2010.
Katika
makala yake, Warner ameendelea kujitetea kwa kusema kuwa, kuishutumu
Afrika Kusini kunachafua hadhi ya hayati Nelson Mandela ambaye
ameisaidia Afrika Kusini kupata nafasi hiyo.
Gazeti
hilo limeonyesha picha za Jack Warner akikutana na Prince William, David
Beckham, Barack Obama na Vladimir Putin ambao amesema wote walikuwa na
ushawishi pindi nchi zao zilipokuwa zikifanya kampeni ya kuwa mwenyeji
wa Kombe la Dunia.Jack Warner amemalizia kwa kuuliza iwapo walikuwa
wanatumia takrima kama rushwa?
Jack
Warner ni mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa bodi ya shirikisho la soka
duniani FIFA, ambao wanatuhumiwa kwa kashfa ya rushwa na mpaka sasa
Warner amekana tuhuma zote zinazomkabili.
No comments:
Post a Comment