RIPOTI YA HALI YA BIASHARA YA MAZAO YA MWAKA 2014 YAZINDULIWA DAR
Naibu
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi (kushoto), akionesha
Ripoti ya Hali ya Biashara ya Mazao yatokanayo na bioteknolojia ya
kisasa ya mwaka 2014 baada ya kuizindua Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia
ni Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa wizara hiyo, Dk.Fidelis Myaka.
Naibu
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi (kulia), akimkabidhi
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Raphael Daluti Ripoti ya
Hali ya Biashara ya Mazao yatokanayo na bioteknolojia ya kisasa ya mwaka
2014 baada ya kuizindua Dar es Salaam leo asubuhi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Mhandisi Raphael
Daluti (katikati), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo. (DK)
Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa wizara hiyo, Dk.Fidelis Myaka (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.
Mtafiti
Mkuu wa Kilimo wa Costech, Dk.Emmarold Mneney (kulia), akitoa mada fupi
kuhusu maendeleo ya bioteknolojia katika uendelezaji wa Sekta mbalimbali
hususan ya kilimo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Maarifa wa Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia (Costech),
Dk.Nicholas Nyange (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo.
Wadau wa sekta ya kilimo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wanahabri wakichukua taarifa hiyo.
Wadau wa sekta ya kilimo wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo.
Waziri Zambi na viongozi wengine wakiwa meza kuu.
Uzinduzi ukiendelea.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Dotto
MwabaleNAIBU Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi amesema
Tanzania haiwezi kukwepa maendeleo ya bioteknolojia katika uendelezaji
wa Sekta mbalimbali hususan ya kilimo.
Kauli
hiyo aliisema wakati akizindua Ripoti ya Hali ya Biashara ya Mazao
yatokanayo na bioteknolojia ya kisasa ya mwaka 2014 baada ya kuizindua
Dar es Salaam leo asubuhi.
" Jukumu
letu ni kushirikiana na wadau wote kuhakikisha tunakuwa na matumizi
salama na endelevu ya bioteknolojia ili kuiondolea wasiwasi jamii kuhusu
dhana iliyopo ya athari zitokanazo na bioteknolojia ya kisasa" alisema
Zambi.
Alisema
kutokana na mantiki hiyo, Serikali imeweka mikakati mbalimbali katika
kushughulikia masuala ya matumizi salama ya bioteknolojia ya mwaka 2010
yenye lengo la kujenga uwezo wa kutumia teknolojia hiyo kwa kuzingatia
faida zilizojidhihirisha katika kuboresha afya ya wanyama na binadamu,
kilimo, viwanda na mazingira.
Zambi
alisema sera ya taifa ya kilimo ya mwaka 2013 inatamka kwamba uelewa
mdogo wa umma kuhusu matumizi ya bioteknolojia unachangia kuwepo kwa
upokeaji mdogo wa teknolojia hiyo kwa madhumuni ya kuongeza matumizi ya
mbinu za bioteknolojia ya kilimo katika uzalishaji, tija na kipato
kwenye sekta ya kilimo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Maarifa wa Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia (Costech),
Dk.Nicholas Nyange alisema teknolojia hiyo mpya ya uzalishaji wa mazao
ni muhimu sana hapa nchini katika sekta ya kilimo.
Mtafiti Mkuu wa Kilimo wa Costech,
Dk.Emmarold Mneney alisema changamoto kubwa waliyonayo watafiti hapa
nchini ni pesa na kuwa wanahitajika kutoka katika utafiti wa ndani na
kutoka nje kama wafanyavyo wenzao wa nchi za Uganda, Kenya ambao tafiti
zao zimefanikiwa katika kilimo cha mahindi, pamba na mohogo.
No comments:
Post a Comment