Burundi yaahirisha uchaguzi wa wabunge

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi
Serikali 
ya Burundi imetangaza kuwa uchaguzi wa rais na wabunge uliotarajiwa 
kufanyika Ijumaa hii umehairishwa mpaka tarehe nyingine itakapopangwa.
Msemaji wa rais Nkurunzinza,Wily Nyamitwe ameiambia BBC kuwa tarehe itapangwa na wasimamizi wa uchaguzi wa nchi hiyo.
Mabadiliko
 hayo yamekuja kutokana na taifa hilo kuingia kwenye machafuko tangu 
Rais Piere Nkurunzinza kutangaza nia ya kuongoza kwa awamu ya tatu baada
 ya kuwa rais kwa miaka 10.
Umoja wa Mataifa imeelezea jinsi mgogoro huo ulivyoongeza idadi ya wakimbizi wanaoikimbia Burundi.
Hivyo kumtaka rais huyo kuachia ngazi mwezi huu kama makubaliano ya Azimio la Arusha yalivyoelekeza.CHANZO:BBC (Muro)
No comments:
Post a Comment