Arturo Vidal wa Juventus kapata ajali.. pamoja na hayo kaingia kwenye matatizo!
Nyota
huyu anatarajiwa kupandishwa Mahakamani hivi karibuni kujibu mashtaka
ya kuendesha gari akiwa ametumia kilevi na tayari amenyang’anywa leseni
yake.
Kiungo wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Chile, Arturo Vidal
amekutwa na huu mkasa ambao huenda atapenda kuusahau haraka
iwezekanavyo wakati akiwa na timu yake ya taifa ambayo kwa mwaka huu
imekuwa mwenyeji wa michuano ya Copa America.
Vidal ambaye
amekuwa kwenye kiwango bora tangu kuanza kwa michuano hiyo akiwa
amefunga mabao matatu kwenye mechi mbili amehusika kwenye ajali ya gari
ambayo imeelezwa kuwa yeye mwenyewe ndio alikuwa chanzo cha ajali hiyo.
Ripoti ya Polisi inaonesha kuwa Vidal alikuwa amelewa wakati akiwa anaendesha gari aina ya Ferarri na alisababisha ajali ambayo ilimsababishia majeraha madogo pamoja na mkewe ambae nae alikuwemo ndani ya gari hiyo.
Wote wawili waliwahishwa hospitalini
ambako wamekuwa wakitibiwa huku hali zao zikielezwa kuwa sio mbaya
kutokana na kupata majeraha madogo kwenye ajali hiyo.
Vidal
alikuwa akitoka kwenye klabu moja ya usiku baada ya wachezaji wa Chile
kupewa ruhusu ya kuondoka kambini baada ya mchezo wao dhidi ya Mexico.
Ripoti zaidi zinasema kuwa Vidal huenda akafukuzwa kambini ikiwa ni moja ya hatua za kinidhamu toka kwa kocha wa timu ya taifa ya Chile, Jorge Sampaoli ikithibitika kuwa aliendesha gari huku amelewa.
No comments:
Post a Comment