TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, May 30, 2015

China yatakiwa kusitisha ujenzi baharini 


Uwanja wa ndege unaojengwa na China katika visiwa vya Spatry
Marekani imetaka kuwepo usitishwaji wa ujenzi wa miradi kwenye maeneo yanayozozaniwa katika bahari ya kusini mwa China.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter aliuambia mkutano mkuu wa ulinzi nchini Singapore kuwa tabia ya China eneo hilio imekiuka sheria za kimataifa
Carter amesema kuwa kuvihami kijeshi visiwa bandia ambavyo vinajengwa na China ni hatua inayoweza kusababisha mizozo ya kijeshi.
Matamshi yake yanakuja siku moja baada ya makao makuu ya jeshi la marekani kusema kuwa china imeweka silaha katika moja ya visiwa hivyo.
Bwana Carter anasema kuwa hakutakuwa na suluhu la kijeshi . Hata hivyo amesema kuwa Marekani itaendelea kuwa na jeshi lake katika eneo hilo.BBC

Muhammadu Buhari atawazwa 

Ukosefu wa usalama, rushwa, uchumi na ajira...hizo ni kama zawadi Goodluck Jonathan (kushoto) anaondoka akimuachia rais mteule wa Nigeria Muhammadu Buhari (kulia). Picha iliyopigwa Mei 28 mwaka 2015.
Ukosefu wa usalama, rushwa, uchumi na ajira...hizo ni kama zawadi Goodluck Jonathan (kushoto) anaondoka akimuachia rais mteule wa Nigeria Muhammadu Buhari (kulia). Picha iliyopigwa Mei 28 mwaka 2015.
Na RFI
Rais mteule wa Nigeria, Muhammadu Buhari, aliyechaguliwa Aprili 1 ameapishwa jana Ijumaa katika mji mkuu Abuja. Wakati huo huo wakuu wapya wa majimbo pia wameapishwa Ijumaa wiki hii.(P.T)
Raia wengi wa Nigeria wana matumaini na Buhuri. Muhammadu Buhari alichaguliwa ili alete mabadiliko katika nyanja mbalimbali nchini Nigeria, licha ya kuwa ni vigumu kukidhi mengi miongoni mwa matarajio.
Mabadiliko ni neno muhimu, hiyo ni kauli mbiu muhimu, Muhammadu Buhari aliyokua akitumia wakati wa kampeni zake za uchaguzi. Afisa huyo wa jeshi mstaafu, ameahidi kutatua matatizo ya ukosefu wa usalama, lakini pia kukomesha umaskini na kutokomeza rushwa.
Lakini pia, timu yake imeanza kugundua, ikiwa ndio mwanzo wa kufanya kazi kwa utawala huo mpya, tatizo kubwa ambalo litawakabili ikiwa ni pamoja na mzigo wa deni la taifa ambalo ni zaidi ya dola bilioni 60, amesema Lai Mohammed, msemaji wa chama cha APC cha Muhammadu Buhari.
" Itabidi tupunguze hali ya maisha na kupitisha sheria kali za bajeti ", amesema Solomon Dalong, mjumbe wa kamati ya mpito ya kuandaa masuala ya haraka ya utawala wa Muhammadu Buhari.
Kamati hii inaamini kwamba rais mpya atafanya kazi kwa haraka kwa sababu, " miaka minne, haitoshi", amekiri mjumbe mwingine wa kamati hiyo.
Hata hivyo rais Buhari atakabiliwa na tatizo la uundwaji wa serikali na ugawaji wa nyadhifa, hasa kuwashirikisha raia kutoka majimbo ya Kaskazini Mashariki ambao walitengwa kwa kipindi kirefu na tawala ziliyotangulia ikilinganishwa na majimbo ya Kusini.

HOTUBA JK KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA 

Ndugu Gratian Mukoba, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania, TUCTA;Mhe. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
Mheshimiwa Gaudencia Kabaka, Waziri wa Kazi na Ajira;
Mheshimiwa Celina Kombani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma;
Mheshimiwa Hamis Majaliwa, Naibu Waziri – TAMISEMI;
Mheshimiwa Margaret Sitta, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi wa Jamii;
Mhe. Felix Daud Ntibenda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha;
Ndugu Msulwa, Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania;
Ndugu Nicholaus Mgaya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania, (TUCTA);
Ndugu Ezekiel Oluoch, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania;(P.T)
Ndugu Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Walimu Tanzania;
Mke wangu Mama Salma Kikwete;
Ndugu Walimu;
Wageni waalikwa;
Shukurani
Nakushukuru sana Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Ndugu Gratian Mukoba na viongozi wenzako wa CWT kwa kunialika na kunipa heshima kubwa ya kufungua Mkutano wenu Mkuu. Nawapongeza kwa maandalizi mazuri ya mkutano. Kufanikisha mkutano wa Wajumbe 1,200 si kazi ndogo hata kidogo. Hivyo basi unapofanikiwa ni jambo linalostahili pongezi. Hongereni sana. Pia nikushukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Arusha na wananchi wote wa Mkoa huu kwa mapokezi mazuri na kwa kukubali kuwa wenyeji wa mkutano huu. Mmekuwa wenyeji wema. Hongereni sana.
Pongezi kwa CWT
Ndugu Rais
Ndugu Waalimu;
Natoa pongezi kwa viongozi wa Chama cha Waalimu wanaomaliza muda wao kwa kazi kubwa nzuri waliyofanya na kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana na yanayoendelea kupatikana. Mmeifanya vyema kazi ya kutetea haki na maslahi ya walimu. Tumejionea jengo kubwa na zuri la kitega uchumi lililojengwa Ilala, Dar es Salaam. Jengo hili lijulikanalo kama Mwalimu House limependezesha sana eneo la Ilala na jiji la Dar es Salaam. Kama kwamba hiyo haitoshi hivi karibuni tumepokea habari nyingine njema za kuanzishwa kwa Benki ya Waalimu itakayojulikana kama Mwalimu Bank. Mafanikio haya na mengine mengi ambayo sikuyataja, yanafanya CWT kuwa moja ya vyama vya wafanyakazi mahiri na makini nchini licha ya kuwa ndicho Chama kikubwa kuliko chote chote. Hongereni sana viongozi na wanachama wa CWT.
Risala ya Chama cha Waalimu
Ndugu Rais
Ndugu Waalimu;
Nimeisikia na kuipokea risala yenu nzuri mliyoiwasilisha kwangu muda mfupi uliopita. Nawashukuru kwa risala yenu imeainisha mafanikio, mliyopata, changamoto zinazowakabili na muhimu zaidi mmetoa ushauri muafaka kuhusu namna bora ya kuzitatua. Ni risala inayotoa fursa ya kujadiliana na kushirikiana na yenye lengo la kujenga na kuimarisha mahusiano ya pande zetu mbili. Ni risala inayoonyesha kuwepo kwa kushirikiana, kustahamiliana na kuaminiana kati ya walimu na Serikali yao. Sisi sote inatupa funzo kuwa, pale panapokuwepo na uhusiano mzuri na ushirikiano kati ya walimu na Serikali, haliharibiki jambo. Hata yale mambo ambayo pengine yalionekana magumu, tumeweza kuyatatua kwa pamoja. Hatuna budi kuendeleza hali hii ya mahusiano kati yetu siku zote.
Risala yenu pamoja na mambo mengine imeibua masuala tisa. Masuala hayo ni kuhusu madaraja ya walimu; posho ya kufundishia; madeni ya walimu; uhaba wa nyumba za walimu; utoaji wa elimu bora; mabadiliko ya mafao ya pensheni; ukaguzi wa shule; Sekta ya Elimu katika BRN; na mapungufu ya kiutendaji katika kuhudumia walimu. Mambo yote haya ni ya msingi sana na yanastahili kupatiwa majawabu muafaka. Yapo ya kisheria, ya kisera na ya kimfumo. Napenda kuwahakikishia kuwa nimeyapokea na tutayafanyia kazi mambo yote kama kawaida yetu. Kama mlivyosema katika risala yenu, baadhi ya mambo yanahitaji kukaa mezani kujadiliana na kushauriana zaidi. Tutafanya hivyo. Nitajitahidi kwa yale yanayowezekana niwe nimeyatatua kabla ya kumaliza muda wangu wa uongozi. Kwa yale ambayo yanahitaji muda mrefu, nitahakikisha kuwa kabla ya kukabidhi ofisi niwe nimeyawekea msingi mzuri ili iwe rahisi kwa Rais ajaye baada yangu kuyakamilisha.
Hatua za Serikali Kushughulikia Madai ya Waalimu
Ndugu Rais na
Ndugu Waalimu;
Kwa uchache, nitapenda kuzungumzia hatua ambazo Serikali imechukua na inazoendelea kuchukua kushughulikia madai ya waalimu. Kama mlivyoainisha katika risala yenu, Serikali ninayoingoza imefanya jitihada kubwa sana kupanua fursa za watoto wetu kupata elimu na sasa tumeelekeza nguvu zetu katika kuboresha elimu inayotolewa. Kwa ajili hiyo, tumeongeza shule za msingi kutoka 14, 257 mwaka 2005 hadi 16, 343 mwaka 2014, na kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka milioni 7.54 hadi milioni 8.23. Shule za Sekondari, zimeongezeka kutoka 1,745mwaka 2005 hadi 4,576 mwaka 2014 na kuongeza wanafunzi kutoka 524, 325 hadi milioni 1.8 kati ya mwaka 2005 na 2015. Hali kadhalika, idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka 26 mwaka 2005 hadi 52 mwaka 2015, na kufanya idadi ya wanafunzi kuongezeka kutoka 40, 719 hadi200, 986 katika kipindi hiko.
Sote tunafahamu kuwa shule na elimu haikamiliki pasipo na waalimu na pasipokuwa vitabu na vifaa vya kujifunzia na kufundishia. Upanuzi huo mkubwa ulilazimu kupanua vyuo vya ualimu. Idadi ya vyuo vya ualimu vya cheti na stashahada vimeongezeka kutoka 52 mwaka 2005 hadi 126mwaka 2015. Upanuzi huu ukiongeza na ule wa vyuo vikuu umewezesha kuongeza idadi ya waalimu wa msingi na sekondari kutoka 153, 767mwaka 2005 hadi 301,960 mwaka 2015. Hii imewezekana kutokana pia na uamuzi wetu wa kutoa mikopo kwa wanafunzi waliochagua kusomea ualimu, na kuwahakikishia ajira pale wanapomaliza masomo yao.
Serikali imefanya jitihada pia za kuboresha maslahi ya waalimu kadri uwezo uliporuhusu. Hatukuweza kutoa nyongeza kubwa kwa wakati mmoja lakini tumeongeza mara kwa mara. Kati ya 2005 – 2015 kumekuwepo na ongezeko la kianzio cha mshahara cha Mwalimu mwenye cheti, Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu na wale wenye elimu ya shahada. Watumishi wa kada nyingine za Serikali wenye elimu ya viwango hivyo, huanza na mshahara wa chini ya ule wa waalimu. Nafahamu kuwa kiwango hiki bado hakitoshi, lakini ukweli ni kuwa hakuna upungufu wa dhamira kwa upande wa serikali, ila kikwazo ni kutokuwepo na uwezo mkubwa kimapato kwa upande wa Serikali. Ukizingatia kuwa walimu ni asilimia 52.7 ya watumishi wa Serikali, hivyo, ongezeko katika mshahara wa waalimu linaleta mabadiliko makubwa sana katika bajeti ya Serikali. Kwa ajili hiyo hatukuweza kutoa nyongeza kubwa kwa wakati mmoja lakini tumeongeza mara kwa mara mpaka tumefikia hapa tulipo leo. Na katika bajeti hii tutaongeza tena. Hivyo nitawaacha mahali penye unafuu ukilinganisha na tulikotoka.
Tumeendelea pia kushughulikia kero nyingine za waalimu ikiwemo madeni na madai yenu. Deni la waalimu lililopokelewa lilikuwa shilingi bilioni 53, 185,440,406 lililohusu waalimu 70,668. Baada ya uhakiki uliofanyika kwa kuhusisha Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani wa Serikali, jumla ya shilingi bilioni 23, 233, 654, 025 zililipwa kwa waalimu 29,243. Serikali imeshatoa ahadi ya kulipa ifikapo mwezi Agosti mwaka huu madai mengine ya waalimu 7,169 yenye jumla ya shilingi bilioni 9, 285,283,600 ambayo uhakiki wake umekamilika. Aidha, madai ya walimu 30,807yenye jumla ya shilingi bilioni 17,346, 593, 468 hayakuweza kulipwa kutokana na kukutwa na dosari za msingi za kihasibu na kiutaratibu. Wametakiwa kurekebisha kasoro zilizoonekana.
Jambo la kururahisha katika ukaguzi na uhakiki huo wa madeni ni kule kushirikishwa kwa Chama cha Walimu. Kwa pamoja tumethibitisha palipokuwa sahihi na pasipokuwa sahihi. Inasikitisha kupata taarifa za kuwepo vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali na walimu vinavyochangia kuzalisha madeni bandia. Vitendo vyao hivyo ndivyo vinavyofanya madai yachukue muda mrefu kulipwa kwa kulazimika kuweko na uhakiki wa ziada. Naungana nanyi katika pendekezo lenu la kutaka watumishi hawa kuwajibishwa, maana ndio mzizi wa fitna kati ya waalimu na Serikali. Nimekwishaeleza mamlaka husika kufanya hivyo bila ajizi.
Ndugu Rais na
Ndugu Waalimu;
Tumeshughulikia lile dai kubwa la waalimu la marekebisho ya muundo wa utumishi wa waalimu (Teacher's Service Scheme). Tumepitisha Muundo mpya wa Waalimu ambao umeanza kutumika toka Julai 1, 2014. Nimesikia kuwa utekelezaji wake haukuweza kuanza kote nchini mara moja, napenda kuwahakikishia kuwa katika mwaka ujao wa fedha tutahakikisha kuwa Waalimu wote watakuwa wamefikiwa. Sambamba na hili la Muundo, tumekwishapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya kuanzisha Tume ya Utumishi wa Waalimu (Teachers Service Commission) ambao tayari umesomwa kwa mara ya kwanza. Mawasiliano yanaendelea na Ofisi ya Spika ili Muswada huo ujadiliwe katika Bunge hili la Bajeti. Tunafanya hivyo pia kwa Muswada wa kuanzisha Bodi ya Taifa ya Taaluma ya Waalimu (Teachers Proffessional Board). Nimepokea maoni yenu ya kutaka uangaliwe uwezekano wa Bodi hii kuwa sehemu ya Tume ya Utumishi wa Waalimu badala ya kuwa na vyombo viwili tofauti. Hoja yenu ya kutaka kupunguza utitiri wa vyombo vinavyoshughulikia maslahi ya waalimu ina mashiko. Ushauri wenu umepokelewa, tutautafakari na kuufanyia kazi.
Napenda kuwahakikishia kuwa madai yenu mengine ikiwemo nyumba za waalimu, motisha kwa waalimu, mazingira ya kufanyia kazi, mafunzo vikokotoo vipya vya pensheni na masuala mengine mliyoibua katika risala yenu tutayashughulikia na tutawapeni taarifa. Pia nitaelekeza mamlaka zinazohusika kukutana na uongozi mpya wa Chama chenu baada ya uchaguzi mkuu wenu kuyajadili masuala hayo na kuyatafutia majawabu.
Napenda kusisitiza kwenu kwamba mimi na wenzangu Serikalini tunawathamini sana na kuwapenda waalimu kwa dhati ya mioyo yetu. Sisi tunatambua nafasi ya Mwalimu katika maendelo ya mtu binafsi na taifa kwa jumla. Hakuna badala yake. Hivyo basi tunatambua wajibu wetu wa kuwawekea mazingira mazuri ya kufanyia kazi. Tumefanya jitihada kutimiza wajibu wetu. Pale panapojitokeza matatizo yoyote si makusudio yetu. Kitendo cha makusudi na anapojulikana mtu huyo atawajibishwa ipasavyo. Wakati mwingine matatizo yanayowakuta hutokana na watu wetu kuelemewa na mzigo kutokana na ukubwa wa kada yenu katika utumishi wa umma ambapo ni asilimia 52. 7.
Kwa ukubwa huu, mnaweza kuelewa ni changamoto kiasi gani zinazojitokeza katika kushughulikia masuala yenu. Ndio sababu hatuchoki kutafuta muundo bora wa kushughulikia matatizo yenu. Ninachoomba kutoka kwenu ni uvumilivu na uelewa wenu na kuwaomba mtupime kwa dhamira yetu na utayari wetu wa kuyashughulikia madai yenu na si kwa idadi ya changamoto zinazojitokeza.
Uchaguzi Mkuu wa CWT
Ndugu Rais na
Ndugu Waalimu;
Moja ya Agenda kubwa ya Mkutano wa leo ni Uchaguzi Mkuu. Nitumie fursa hii kuwapongeza viongozi mliochaguliwa katika ngazi ya Tawi, Wilaya na Mkoa ambao kwa pamoja mmeunda Mkutano Mkuu huu. Nawapongeza kwa kuuendesha uchaguzi wa ngazi za chini vizuri maana natambua kuwa haikuwa kazi ndogo kutokana na ukubwa wa nchi yetu, na hamasa ya waalimu kisiasa.
Nawapongeza sana viongozi wote waliojitokeza kugombea nafasi za uongozi wa ngazi ya Taifa. Naamini nyote mnatosha kwa nafasi mnazoomba. Naomba mkumbuke kuwa si kila mtu aliyeomba atashinda. Nafasi si nyingi kiasi hicho. Hivyo basi, wale ambao kura hazitatosha safari hii, watumie uzoefu walioupata katika uchaguzi huu kujinoa zaidi kwa chaguzi za miaka ijayo. Haitakuwa vizuri iwapo wale ambao hawatafanikiwa kushinda, wataendeleza nongwa na kuwa chanzo cha kuvunja mshikamano mzuri mlionao katika Chama cha Walimu. Kama nilivyosema awali, sisi sote tunawaangalia waalimu kama kioo cha maadili na upevu katika jamii yetu. Naamini hamtatuangusha.
Nawapongeza na kuwashukuru sana viongozi wanaomaliza muda wao kwa ushirikiano wenu mkubwa mliotupatia sisi katika Serikali katika kipindi chenu cha uongozi. Kwa pamoja tumeweza kutatua changamoto nyingi za waalimu na kujenga madaraja kati yetu yaliyozaa mahusiano mazuri ambayo ndio msingi wa kutatua madai ya waalimu kila yalipojitokeza. Ni matumaini yetu kuwa viongozi watakaochaguliwa, wataendeleza pale mlipoishia na muhimu zaidi uhusiano mzuri na ushirikiano na Serikali. Sisi tunaahidi kuwapa kila aina ya ushirikiano unaostahili. Ni jambo lenye maslahi kwetu sote.
Hitimisho
Ndugu Rais na
Ndugu Waalimu;
Hii ni fursa yangu ya mwisho kukutana na kuzungumza na viongozi wa CWT nikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya hapo nitakuja kumsindikiza Mwalimu mwenzenu akija mkutanoni. Hivyo, sina budi kutumia fursa hii pia kuagana nanyi na kupitia kwenu kuagana na Waalimu wote nchini. Nirudie tena kuwashukuru sana kwa mchango wenu mkubwa katika maendeleo ya elimu nchini. Kwa kweli mnajitoa sana na mnafanya kazi kubwa ambayo inaonekana na wote. Napenda kuwatia moyo kuwa msilegeze uzi bali muendelee na moyo na wito wenu huo. Nitawakumbuka sana waalimu katika maisha yangu baada ya kustaafu uongozi, kwa msaada wenu na ushirikiano wenu. Nimewapenda, ninawapenda na nitaendelea kuwapenda 'Shemeji' zangu.
Nawatakia Uchaguzi Mkuu na Mkutano Mkuu mwema.
Akhsanteni kwa kunisikiliza!

Friday, May 29, 2015

Hivi ndio visiwa kumi vyenye mvuto zaidi duniani… Afrika kiko kimoja tu, ni TZ au? (Pichaz)

madeira
Nimeona nikusogezee pichaz za hivi visiwa 10 ambavyo viko kwenye list ya vinavyoongoza kwa kuwa na mwonekano mzuri zaidi duniani.. Afrika tunawakilishwa na kimoja, unadhani kitakuwa ni cha TZ?
pro
1. Providenciales – Uturuki
maui
2. Maui – Marekani
roatan
3. Roatan – Honduras
santo
4. Santorini – Ugiriki
koh
5. KO TAO – THAILAND
madeira
6. Madeira – Ureno
madeira
bali
7. Bali – Indonesia
mau
8. Mauritius
bora
9. Bora Bora- French Polynesia
nooo
10. Fernando De Noronha- Brazil

SERIKALI YASHAURIWA KUONGEZA BAJETI WIZARA YA HABARI 

01
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo leo bungeni mjini Dodoma.
02
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Said Mtanda akiwasilisha mapendekezo ya kamati yake kuhusu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa bajeti ya wizara hiyo leo mjini Dodoma.
03
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kutoka kushoto) wakifuatilia kwa makini bajeti ya Wizara hiyo leo mjini Dodoma. (DK)
04
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma.
Serikali imeshauriwa kutenga fedha za kutosha ili kuiwezesha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Ushauri huo umetolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakati wa kuwasilisha mapendekezo yake leo bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati Mhe. Said Mtanda amesema Wizara hiyo ina jukumu la kuratibu na kusimamia maendeleo ya vijana, utamaduni, michezo na habari hivyo ikipewa fungu la kutosha itaweza kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta hizo.
Akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake bungeni leo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara ameliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya wizara hiyo ya shilingi bilioni 29.4 ambapo shilingi bilioni 5 ni kwa ajili ya maendeleo na shilingi bilioni 24.4 ni matumizi ya kawaida.
Aidha Waziri Mukangara ameeleza jitihada mbalimbali zinazofanywa na wizara yake zikiwemo kuratibu na kuwajengea vijana uwezo wa kubuni mawazo bora ya kujiajiri, kuhamasisha halmashauri kutenga asilimia 5 ya bajeti yao kuboresha mifuko ya vijana na kuhamasisha uanzishaji wa SACCOS.
Katika mwaka wa fedha uliopita wa 2014/2015, Waziri Mukangara amesema wizara yake ilitoa mafunzo kwa vijana 1550 katika kujenga dhana ya kujiajiri, na jumla ya shilingi bilioni 2 zilikopeshwa kwa vikundi mbalimbali vya vijana kote nchini.
Kwa upande mwingine Dkt Mukangara amesema wizara yake imekamilisha miradi kadhaa ukiwemo mradi wa Mawasiliano na kukamilisha lengo la milenia la kubadili matumizi ya analojia kwenda dijitali, mradi huo ulikamilika mwezi Aprili mwaka huu. Miradi mingine katika mwaka wa fedha uliopita ilikuwa ni ya utafiti ukiwemo wa msamiati wa lugha za jamii, utafiti wa majina fiche 1800 ya lugha za asili.
Wizara katika mwaka huu wa fedha imeahidi kuongeza ufanisi ikiwemo kuongeza ajira kwa vijana, kulinda mazingira, kutoa habari, kulinda mila na desturi kudumisha amani na mshikamano wa katika jamii ya watanzania.
Leo ni siku ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo zimewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara zao na hatimaye kuruhusu Bunge kuendelea kuzijadili bajeti hizo.
mitambo ya kukodi TBC na uchaakavu wa majengo, madeni 3.2 /1.3 serikali.
Katika kipindi cha 2014/15 wizara ipanga kukusanya sh. 1,149,008,000 kutoka vyanzo mbalimbali zilizokusanywa ni sh. 811,616,116 sawa 71%
Wizara ilitengewa (2014/2015) 19,806,611,000 zilipokelewa sh. 14,446,963,490 sawa na 73% ya bajeti ya matumizi ya kawaida. Fedha za maendeleo wizara 2014/15 ilitengewa 16,850,000,000 ilipokea hadi april 2015 >7,000,000,000 sawa 42% upanuzi wa usikivu wa shirika la utangazaji la Tanzania TBC
Moja ya changamoto ni kuongezeka kwa mifumo na njia za mawasiliano kwa umma kama mitandao ya jamii kwenye intanet kunakoadhiri maudhui ya taarifa zinazotolewa
Wizara kukabiliana na changamoto hizo imetoa elimu na kutembelea vituo kwa kushirikia na kamati ya maudhui (TCRA)

Watumishi Bodi ya Mikopo watakiwa kuongeza ufanisi 

Nyatega RAAWU 2
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. George Nyatega (mwenye tai) akipokea tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (RAAWU) – Tawi la HESLB Bw. Deodatus Mwiliko kutambua uongozi wake bora katika HESLB tangu ilipoanzishwa mwaka 2005. Wengine ni viongozi wa RAAWU-HESLB Bw. Luhano Lupogo na Bi. Octavia Selemani. (Picha na HESLB).
Nyatega RAAWU 1
Na Mwandishi wetu
Watumishi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wametakiwa kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuondokana na malalamiko kutoka kwa wanafunzi.(P.T)
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega ametoa wito huo mara baada ya kukabidhiwa tuzo naChama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (RAAWU), tawi la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Akiongea katika hafla fupi ya kukabidhi ngao hiyo, Mwenyekiti wa RAAWU Tawi la HESLB Bw. Deodatus Mwiliko alisema RAAWU, Tawi la HESLB imeamua kumkabidhi Mkurugenzi mtendaji huyo ngao hiyo kutokana na kujali na kuboresha mazingira ya kufanya kazi kwa watumishi wote wa HESLB.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema amepokea tuzo hiyo kwa niaba ya menejimenti anayoingoza na wafanyakazi wote na kuwataka watumishi wa HESLB kutoridhika na ufanisi uliopo na badala yake waongeze juhudi.
“Ninapokea hii ngao kwa niaba ya menejimenti na wafanyakazi wote kwa sababu sifanyi kazi peke yangu,” alisema Bw. Nyatega jana (Alhamisi, Mei 28, 2015) katika makao makuu ya HESLB jijini Dar es Salaam.
“Ninawapongeza kwa kufanya kazi kwa ufanisi, lakini pia muongeze juhudi katika utoaji wa huduma kwa wanafunzi ili pasiwe na malalamiko,” amesema Bw. Nyatega.
HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Tangu kuanzishwa kwake, Bw. Nyatega amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wake.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu AWASILISHA BAJETI YAKE BUNGENI MJINI DODOMA-MEI 28,2015 

4
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na Waziri kivuli wa Maliasili na Utalii, Peter Msingwa kabla ya kuasilisha bajeti yake bungeni.
5
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiwasilisha bajeti bungeni mjini Dodoma.
8
 Lazaro Nyalandu akiondoka baada ya kumaliza kusoma bajeti yake. (DK)
1
Baadhi ya mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
7
Baadhi ya askari wa wanyamapori wakifuatlia hotuba ya bajeti bungeni.
2
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na naibu wake Mahmood Mgimwa bungeni.
3 
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akisalimiana na baadhi ya wabunge bungeni.

Thursday, May 28, 2015

MKUTANO WA KANDA YA AFRIKA WAFANYIKA MJINI ABIDJAN 

4
Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servcius Likwelile akiwaeleza Mawaziri wa Fedha kuhusu serikali ya Tanzania mipango yake hasa kwenye miundombinu. Kutoka kulia ni Waziri wa Fedha wa Rwanda Bw. Claver Gatete na kushoto kwake ni Mchumi Mkuu Rugwabiza Minega Leonard. ilivyonufaika na fedha za Benki ya Maendeleo katika kutekeleza.
3
Waziri wa Fedha wa Rwanda Mhe. Claver Gatete akitoa ufafanua wa masuala mbalimbali yanayohusu nchi za Afrika. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile ambaye amemwakilisha Waziri wa fedha na kulia kwake ni Waziri wa Fedha wa Ethiophia Mhe. Fisseha Aberra.
5
Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi kuhusu Tanzania inavyoshirikiana na Benki ya Afrika kwa Mawaziri wa Fedha kutoka nchini Rwanda, Ethiophia, Kenya na Visiwa vya Shelisheli wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya utekelezaji wa mazimio ambayo kila nchi imejiwekea.
1
Kamishna wa Fedha za Nje Bwana Ngosha Manyoga akiwa katika majadiliano yanayohusu ya ripoti ya utekelezaji wa mpango wa mafanikio katika nchi za Africa.(VICTOR)

TUZO YA BBC:HEKO KWA ASISAT OSHOALA 

150526152603_oshoala_premio_bbc_640x360_bbc_nocredit
Mshambuliaji wa Nigeria na timu ya Wanawake ya Liverpool, Asisat Oshoala ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya BBC ya mwanasoka bora wa mwaka.
Oshoala, mwenye umri wa miaka 20 ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo mpya kutoka BBC World Service,kwa kura zilizopigwa na wapenzi wa kandanda duniani.
Mwanadada huyu amemuangusha Veronica Boquete wa Uhispania na Nadine Kessler wa Ujerumani,Scot Kim Little na Marta wa Brazil.
"ninapenda kutoa shukrani zangu kwa BBC,mashabiki wangu duniani na kila mmoja aliyepiga kura" alisema.
Tuzo hii ni ya kwanza kufanyika na Shirika la utangazaji la kimataifa.
Oshoala, ambaye ni mchezaji mwenye umri mdogo kuliko wote kati ya wapinzani wake, alikuwa mfungaji bora na alipigiwa kura wakati wa michuano ya kombe la dunia la wachezaji wa umri wa chini ya miaka 20 nchini Canada kipindi cha majira ya joto kilichopita.
Jitihada zake ziliifikisha Nigeria katika hatua ya Fainali ambapo ilikutana na Ujerumani, ambapo Ujerumani ilipata ushindi mwembamba dhidi ya Nigeria.
Pia alitoa mchango mkubwa katika timu ya wanawake ya Nigeria katika kutwaa ushindi wa kombe la mabingwa Afrika kwa wanawake mwezi Oktoba.
Hatua hiyo imeiwezesha Nigeria kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia kwa wanawake nchini Canada inayoanza tarehe 6 mwezi Juni
CHANZO:BBC
IMECHOTWA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON

Wednesday, May 27, 2015

Akon kaliona tatizo la umeme kwenye nchi za Africa, ameamua kujitolea !!

AKON-LOGO1

Jina la Aliaune Damala Badara Thiam labda ni gumu kumjua huyu ni staa gani wa muziki duniani.. okay, jina lake kwenye stage ni Akon, Msenegal aliyetoboa anga na kufanikiwa kutengeneza mafanikio makubwa kupitia muziki duniani akiwa kwenye ardhi ya Marekani !!
Akon alikuwa Kenya mwezi mmoja uliopita kwenye fainali za Trace Music Star, ikawa furaha kwetu kumuona Mayunga wetu kaibuka mshindi.. safari inaendelea kati ya Mayunga na Akon kwenye muziki, tutarajie chochote kikubwa zaidi kupitia kinachoenda kufanyika marekani.
Ishu ambayo nimeona nikusogezee ni kuhusu Akon mwenyewe.. kwa sasa jamaa kaamua kuwekeza mamilioni ya pesa zake kwenye miradi ya solar energy Africa, watu zaidi ya milioni 600 watanufaika na mradi huu.
Ndani ya mwaka mmoja nchi ambazo zitakuwa zimeshanufaika na mradi huu ni Mali, Guinea, Benin, Senegal, Niger, Gabon, Equatorial Guinea, Congo-Brazzaville, Kenya, Sierra Leone na Burkina Faso.
Mradi huu umepewa jina la Akon Lighting Africa,
United

Akon II akon

Kikao na mapendekezo ya majimbo mapya ya uchaguzi Dar 

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akiongoza kikao cha RCC, Ilala Boma jijini Jumanne Mei 26, 2015.
Kikao kilichowaleta pamoja Wabunge wote wa Dar es Salaam, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Manispaa zote tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni, Watendaji wa Manispaa hizo, na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, kimependekeza kuongezwa kwa majimbo zaidi ya uchaguzi kwenye jiji hilo lenye wakazi wanaokaribia milioni tano.
Majimbo pendekezwa waliyataja kuwa ni Kijichi wilayani Temeke, Chanika wilayani Ilala, Bunju na Kibambawilayani Kinondoni.
Mapendekezo hayo uatapelekwa tume ya taifa ya uchaguzi (NEC), kwa uamuzi wa mwisho.(P.T)

Majeshi ya Hamas yalaumiwa kwa ukatili 

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limelaumu majeshi ya Hamas huko Gaza kwa kuendesha vitendo vya kikatili na utekaji nyara, mateso na mauaji kwa raia wa kipalestina kufuatia mgogoro kati ya Israel na makundi ya wapiganaji wa Palestina katika maeneo ya mpakani.
Mashambulio hayo yaliwalenga raia wakiwatuhumu kushirikana na Israel.
Amnesty imesema kwamba hali ni mbaya wakati vikosi vya askari wa Israel wakiwa katika harakati zao za mauaji ya kutisha na uharibifu kwa watu wa Gaza,Hams inatumia fursa hiyo kujipanga kwa ushindi.BBC
Ripoti hiyo inabainisha kuwa harakati za chama cha Hamas ambacho kimekuwa kikiaminiwa inaonyesha kuwa imekuwa ikitumia mashambulizi ya majeshi ya Israel kulipiza kisasi dhidi ya maadui ndani ya chama hicho.
Wapalestina wapatao 23 kwa mjibu wa ripoti hiyo wameuawa kinyama huku mamia wakifungwa na kuteswa, wakiwemo wanachama wa chama cha upinzani kinachoipinga Hamas chama cha Fatah.
Hamas imekuwa ikiwalaumu maadui zake kuwa wamekuwa wakishirikiana na Israel ambapo ripoti hiyo inabainisha kuwa wengi ya waliouawa ni wale waliokuwa wamefungwa gerezeni wakati wa mgogoro ulioibuka hivi karibuni, ambapo baadhi yao waliuawa kinyama hata kabla ya kesi zao kumalizika.
Katika tukio moja la kushitua wanaume sita waliuawa kwa kupigwa risasi nje ya Msikiti walipokuwa wamepiga magoti mbele ya umati wa watu wakiwemo wanaume wanawake na watoto.
Ripoti hiyo ya Amnesty inawashutumu Hamas pia kwa madai ya kupanigia haki na uhuru kwa wapelestina wakati wao wamekuwa hawafanyi mambo yanayofanana na yale wanayoyasema.
Shirika la Amnesty limeitaka Hamas kushirikiana na Tume ya uchunguzi ya kimataifa inayochunguza ukiukwaji huo wa haki za binadamu na kuwafikisha wote waliohusika kwenye mkono wa sheria.

Madagascar : wabunge wapiga kura ya kujiuzulu kwa rais 

Rais wa Madagascar, Hery Rajaonarimampianina, Januari mwaka 2014.
Rais wa Madagascar, Hery Rajaonarimampianina, Januari mwaka 2014.
Na RFI
Mvutano wa kisiasa umejitokeza nchini Madagascar. Wabunge 121 kwa jumla ya wabunge 125 walioshiriki kikao cha Bunge Jumanne wiki hii, wamepiga kura ya kujiuzulu kwa rais wa nchi hiyo Hery Rajaonarimampianina, mwaka mmoja na nusu baada ya kuchaguliwa kwake kuliongoza taifa hilo.
Wabunge hao wanamtuhumu rais Hery Rajaonarimampianina kwamba amekiuka katiba ya nchi. Rais huyo anaonekana kupoteza imani kwa wabunge hao.
" Hajui majukumu yake, hawezi kuliongoza taifa la Madagascar ", wamesema baadhi ya wabunge. Tuhuma hizo dhidi ya rais Hery Rajaonarimampianina zimeibuka katika kikao cha Bunge cha Jumanne jioni wiki hii, ambapo kikao hicho kiligubikwa na mvutano. Baada ya kikao, baadhi ya wabunge walitaka kuzipiga, na hali hiyo ikapelekea wanajeshi wanaolinda jengo la Bunge kuingilia kati ili kuzuia rabsha isitokei.(P.T)
Wakiwa na hasira, wabunge hao wamemkosoa rais kwamba hana uamzi katika majukumu yake. Ilimpasa zaidi ya miezi miwili ili kupata waziri mkuu, kabla ya kumfuta kazi baada ya miezi minane. Mahakama Kuu ambayo ingeliundwa katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya uchaguzi wa rais haijaundwa. Herry Rajaonarimampianina pia anatuhumiwa kujaribu kushawishi kazi ya wabunge.
Kazi kubwa kwa Mahakama Kuu ya Katiba
Lakini hasira za wabunge zililipuka baada vikao vya kuboresha Maridhiano, vilivyohitimishwa wiki tatu zilizopita. Hakuna mbunge aliyealikwa miongoni mwa washiriki 2,000 waliohudhuria vikao hivyo. Na kuvunjwa kwa Bunge ilikuwa miongoni mwa mapendekezo ya mwisho ya vikao hivyo. Kura iliyopigwa Jumanne wiki hii ina kinga fulani kwa wabunge.
Mahakama ya Katiba (HCC) na majaji wake tisa ndio wana majukumu ya kuthibitishwa au la kwa kujiuzulu katika siku zijazo kwa rais huyo.
Herry Rajaonarimampianina bado ni rais mpaka pale uamzi wa Mahakama ya Katiba wa kujiuzulu kwa rais huyo utatolewa. Inasemekana kuwa majaji wa Mahakama ya Katiba ni washirika wa karibu wa utawala.

JK AFUNGUA MKUTANO WA MABALOZI WA TANZANIA.

1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wakati wa mkutano wa mabalozi wa Tanzania.Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,unaojadili kwa kina namna ya kutekeleza dira mpya ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania ili kuendana na mabadiliko ya Uchumi na Diplomasia Duniani na kuleta tija nchini. (Watatu Kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje Mh.Bernard Membe,Wanne kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Liberata Mulamula.(VICTOR)

MIZENGO PINDA AJIANDIKISHA KIJIJINI KWAKE 

index
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Watanzania wote watumie fursa ya uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura kwa kujiandikisha ili waweze kushiriki uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kujiandikisha kwenye Ofisi ya Mtendaji Kata iliyopo kijiji cha Kibaoni, wilayani Mpanda, mkoani Katavi jana jioni (Ijumaa, Mei 25, 2015), Waziri Mkuu alisema hii ndiyo fursa pekee ya kuwawezesha kushiriki uchaguzi mkuu ujao.
"Ninawasihi Watanzania wote tusiache kutumia fursa hii... kila mtu ahakikishe kuwa anajiandikisha. Ni fursa pekee itakayohakikisha kila mwananchi anashiriki uchaguzi wa kumpata Rais, Mbunge na Diwani," alisema.
Waziri Mkuu alisema amefarijika kwa kazi aliyoiona ikifanyika kwani hadi sasa Halmashauri za Nsimbo na Mlele zimefanikiwa kuandikisha watu kwa zaidi ya asilimia 100.
Mapema, akiwasilisha taarifa ya uandikishaji katika Halmashauri ya Mlele, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw. Godwin Benne alisema walilenga kuandikisha watu 19,482 lakini hadi kufikia jana walifanikiwa kuandikisha watu 20,292 sawa na asilimia 105. Uandikishaji katika wilaya ya Mlele ulianza tarehe 18 Mei, mwaka huu.
"Mlele tuna vituo 84 katika tarafa tatu za Inyonga, Mpimbwe na Mamba. Inyonga tuna vituo 28, Mpimbwe viko 23 na Mamba viko 33.
Akifafanua zaidi, Bw. Benne alisema katika kata ya Kibaoni ambayo ina vituo sita, jana peke yake walifanikiwa kuandikisha watu 1,007 kikiwemo kituo cha Kibaoni ambacho Waziri Mkuu Pinda alijiandikisha. Alivitaja vituo vingine kuwa ni Milumba, Sungusungu, Ilalangulu, Manga na Shule ya Msingi Kakuni ambako Mama Tunu Pinda alijiandikisha jana hiyo hiyo.
Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Bw. Neneka Rashid, uandikidhaji ulianza Mei 18, 2015 kwenye kata 12 na kwamba hadi kufikia jana, kata nne zilikwishaandikisha watu 12,001 sawa na asilimia 108.9 licha ya kuwa matarajio yao yalikuwa ni kuandikisha watu 11,014. Alizitaja kata hizo kuwa ni Nsimbo, Kapalala, Magamba na Uruwira.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MEI 26, 2015.
(VICTOR)

SERIKALI YAMKARIBISHA MWAKILISHI MKAZI MPYA WA JICA NCHINI

2
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi (kulia) na aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (wa pili kutoka kulia) katika hafla fupi ya kumuaga Bw. Shinya iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.Wengine ni Afisa Tawala Msaidizi wa JICA Bw. Nasibu Hamisi (wa tatu kutoka kulia) na Afisa Tawala wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi. Mwanamridu Jumaa (wa nne kutoka kulia).
3
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi (kushoto) alipoitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.
5
Kaimu katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akimkabidhi zawadi Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA nchini aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (kulia) katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.(VICTOR)

Tuesday, May 26, 2015

Mkutano wa Dharura Nchi za EAC kuhusu Burundi kufanyika mwishoni mwa mwezi Mei

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) tarehe 25 Mei, 2015 kuhusu Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2015 kuhusu masuala ya amani na usalama nchini Burundi. Mkutano huo ambao umeitishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya EAC, Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete utatanguliwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri.

Mhe. Membe akiendelea na mkutano wake na Waandishi wa Habari.Picha na Reginald Philip.(Muro)

UPENDO NKONE, MIKE KALAMBAY WANOGESHA TAMASHA LA GOSPEL COLUMBUS, OHIO 


Mwimbaji wa nyimbo za injili wa Columbus, Ohio Enock Mwamba(kati) akiimba moja ya nyimbo za injili huku akiwashirikisha Mike Kalambay aliyekuja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Upendo Nkone aliyekuja toka Tanzania maalum kunogesha tamasha la Gospel lililofanyika siku Jumapili May 24, 2015 na kuhitimisha tamasha hilo lililokua la siku 3 mjini humo lililoanzia siku ya Ijumaa May 22, 2015.

Mike Kalambay akiimba moja ya nyimbo za injili kwenye tamasha la gospel lililofanyika siku ya Jumapili May 24, 2015 mjini Columbus, Ohio.

Mike Kalambay toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akishambulia jukwaa na nyimbo za injili.

Mwimbaji mahili wa nyimbo za Injili Upendo Nkone akiimba moja ya nyimbo zake kwenye tamasha hilo.(Muro)