WAJUE MABILIONEA WATANO WA TANZANIA
WAFANYABIASHARA watano, Said Bakhressa Gulam Dewji, Rostam Aziz,
Reginald Mengi na Ali Mufuruki, wametajwa na Jarida la Ventures Africa
linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika kuwa ndiyo
matajiri zaidi nchini.
Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa
anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni
sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye
utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni). Wengine na kiasi cha
mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola
420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176
bilioni - Dola 110 milioni).
Matajiri hao wamepatikana baada ya kuangalia nafasi zao kifedha, ufanisi wa kampuni zao katika soko la hisa, mfumo wa wanahisa katika soko la hisa na mtiririko mzima wa fedha katika akaunti zao kwenye benki mbalimbali. Jarida hilo linalotoka mara moja kwa mwezi kutoka Afrika Magharibi, limesema matajiri hao wa Tanzania ni kati ya Waafrika wenye utajiri ambao ni mabilionea 4,800 kutoka mataifa 17.Asilimia kubwa ya watu 1,523 ni mamilionea na wamo katika ripoti ya watu matajiri Afrika.Jarida hilo linataja jinsi matajiri hao walivyokuwa wajasiriamali wadogo kabla ya kuibuka na kuwa mabilionea.
Soma zaidi...http://www.mwananchi.co.tz/habari
No comments:
Post a Comment