TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, November 22, 2012

MAWAZIRI WAZOMEWA MBELE YA KINANA






















 Na: Abdallah Bakari, Mtwara na Raymond Kaminyoge, Sumbawanga

MAWAZIRI watatu wa Rais Jakaya Kikwete juzi walizomewa baada ya kupanda jukwaani kujibu kero mbalimbali za wananchi katika mkutano wa kwanza wa viongozi wapya wa CCM taifa, ulioongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahaman Kinana.

Tukio hilo lilitokea juzi mkoani Mtwara ambako Kinana na mawaziri hao walikuwa katika ziara ya chama kujibu kero mbalimbali za wananchi.Mawaziri waliokumbwa na dhahama hiyo ni Christopher Chiza wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Hawa Ghasia (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Tamisemi) Naibu wake, Aggrey Mwanri.

Chiza ndio alikuwa wa kwanza kukumbana na zomeazomea hiyo, lakini mambo yalikuwa magumu zaidi kwa Ghasia ambaye alizomewa tangu alipoanza kuzungumza mpaka alipomaliza.Ghasia ambaye pia ni mbunge wa Mtwara Vijijini, alirushiwa makombora na Rukia Ismail Athumani ambaye alimshutumu yeye pamoja na Mbunge wa Mtwara mjini, Asnein Murji kwamba waliruhusu gesi kupelekwa Dar es Salaam wakati wananchi wa mkoa huo hawajafaidika nayo.

“Ghasia na Murji kwanini mnaudanganya umma kwa kupeleka gesi Dar es Salaam, sisi hatuna ubaya na chama ila hatutaki gesi iende huko” alisema Athumani huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo.Kabla ya dada huyo kuteka hisia za wananchi kwa kuwasilisha kero hiyo, Kinana alimruhusu mwananchi mwingine, Issa Kambona ambaye pia alieleza kuwa hakubaliani na suala la gesi hiyo kupelekwa Dar es Salaam.

Kinana alisema amesikia hoja hizo za wananchi na kwamba atamueleza Waziri wa Nishati na Madini azungumze na wananchi wa Mtwara kuhusu gesi hiyo.Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu, Ghasia alilazimika kupanda jukwaani kujibu makombora aliyokuwa akirushiwa na wananchi waliofika katika mkutano huo.

“Sio kweli kwamba hatutetei maslahi yenu, gesi iliyopo ni... Soma zaidi... http://www.mwananchi.co.tz, chanzo gazeti la mwananchi

No comments:

Post a Comment