HOSPTALI 37 NCHINI KUNUFAIKA NA BILION YA UHOLANZI
Balozi wa Uholanzi nchini Dr. Ad Koekkoek (kulia) akitoa ufafanuzi
kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusu msaada wa shilingi
bilioni 33 uliotolewa na Uholanzi kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili kuimarisha
huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali katika Hospitali 37
hapa nchini . Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah.
Tanzania nayo inatakiwa kuchangia kiasi kama hicho katika huduma hiyo ili
kuwa asilimia 50 kwa 50 kila pande yaani Tanzania na
uholanzi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) na Balozi wa Uholanzi
nchini Dr. Ad Koekkoek (kulia) wakibadilishana hati
ya msaada wa shilingi bilioni 33 uliotolewa na Serikali ya
Uholanzi kwa Serikali ya Tanzania
TANZANIA
imepokea msaada wa shilingi bilioni 33 kwa ajili kusaidia uboreshaji wa huduma
za uchunguzi wa afya kwa kipindi cha miaka mitano ijayo hapa
nchini.
Msaada huo
huo utawezesha Serikali ya Tanzania kuboresha huduma ya uchunguzi katika
hospitali 37 kwa ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kufanyia uchunguzi ambavyo
vitawasaidia wataalam kutoa matokeo ya matatizo yanayowakabili wagonjwa kwa haraka
zaidi .
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dar es
salaam mara baada ya kupokea msaada huo kutoka Ubalozi wa Uholanzi hapa nchini
kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan
Khijjah alisema msaada huo utaiwezesha Serikali
kunulia vifaa vya kufanyia uchunguzi wa kisasa kama vile kununulia vifaa vya
X-ray na ultrasound ambazo vitasambazwa katika
Hospitali hizo
Alisema
kuwa msaada huo ni muhimu kwa Serikali ya Tanzania kwani
utaisaidia Serikali kupunguza gharama ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa wale
wanaohitaji kupatiwa huduma za uchunguzi wa kina wa afya zao
badala yake kazi itafanyika hapa nchini mara baada ya ununuzi wa
vifaa hivyo.
Khijah
alisema katika makubaliano Serikali ya Tanzania nayo itachangia kiasi hicho
fedha katika msaada huo ili kufanikisha ununuzi wa vifaa vya huduma ya uchunguzi
.
Alisema
kuwa msaada huo utadumu kwa kipindi cha miaka mitano ambapo mara baada ya miaka
hiyo kumalizika Serikali ya Tanzania itasimamia yenyewe
.
Alitaja mikoa itakayonufaika na msaada huo
ni pamoja na Shinyanga, Kagera, Iringa, Mwanza, Pwani, Lindi,
Mtwara, Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Kigoma, Manyara, Mbeya, Morogoro,
Kilimanjaro, Mara, Rukwa, Singida, Ruvuma, Tanga na Tabora. Kufuatia
hali hiyo Katibu Mkuu huyo aliwataka watendaji wa Hospitali zote zitakazonufaika
na msaada huo kuwa makini katika utunzaji wa vifaa ili viweze kutumika kwa muda
mrefu na uboreshaji wa afya za wananchi.
Naye Balozi wa Uholanzi nchini Dkt. Ad Koekkoek alisema kuwa msaada
huo unalenga upatikanaji wa huduma za bora za ultra sound, CT scan ,na x-ray
hapa nchini na hivyo kuboresha huduma za afya.
Aliongeza kuwa huduma hiyo inalenga kuufanya uchunguzi wa magonjwa
uwe wa kisasa zaidi ambapo wataalam wataweza kufanya uchunguzi kwa haraka na
kama kama utahijika sehemu nyingine kuweza kuutuma kwa njia
mtandao(internet).
No comments:
Post a Comment