TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, November 13, 2012

MABANGO YENYE USO WA RIHANA ULIOJERUHIWA MWAKA 2009 YATUMIKA KUPINGA SHOW YA CHRISS BROWN SWEEDEN
Rihanna anaweza kuwa ameshamsamehe Chris Brown kwa kumpiga miaka mitatu iliyopita lakini kuna watu mjini Stockholm, Sweden bado hawajamsamehe.

Kwa mujibu wa website moja ya nchini Sweden, Alour se, mabango yenye picha ya mpenzi wake wa zamani na Chris zinazoonesha alivyojeruhiwa usoni kutokana na kipigo hicho yamebandikwa kwenye mitaa kadhaa mjini humo kupinga show yake ya November 19.


Chris bado yupo kwenye probation kwa miaka miwili mingine kutokana na kumpiga vibaya Rihanna mwaka 2009. Chris na Rihanna hivi karibuni wamerudisha urafiki wao kiasi cha Breezy kumpiga chini mpenzi wake Karrueche Tran ili tu kuwa karibu na muimbaji huyo wa Diamonds.

Kwa mujibu wa interview ya hivi karibuni kupitia Facebook Live Chat na Andy Cohen Rihanna alisema hana uhusiano wa kimapenzi na Chris.

No comments:

Post a Comment