TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, November 7, 2012

MALAWI KURUHUSU NDOA ZA JINSIA MOJA !

























Serikali ya Malawi imesitisha rasmi mswaada wa sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja na polisi wameagizwa kutowakamata watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga mpaka uamuzi mwingine utakapotolewa.
Mapenzi ya jinsia moja kwenye nchi ya Malawi yalipigwa marufuku na kutolewa kifungo cha miaka 14 jela kwa wanaokamatwa kushiriki na siku kadhaa zilizopita baadhi ya viongozi wa kimagharibi wametishia kusitisha kuzipa msaada nchi za Afrika ambazo zinakataa kutambua haki za mashoga.
Mmoja wa viongozi wa kijamii mwenye ushawishi mkubwa anaeitwa Kaomba, amiomba serikali kutoruhusu bunge kubadili sheria zake kuhusu ushoga huku akisema ni kinyume na maadili.
BBC Swahili wamesema mwandishi wao ambae yuko Blantyre anasema kuwa kusitisha kwa muda sheria hiyo, kutawaudhi sana watu wengi hasa viongozi wa kidini pamoja.
Kama unakumbuka… mwaka 2010 wanaume wawili walikamatwa na kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu hadharani baada ya kusema wataoana ambapo hiyo kesi ilikua kero kwa mataifa yanayosupport hizo ndoa za jinsia moja na hata kusababisha baadhi yao kusitisha msaada kwa Malawi, na ikawa pigo kubwa kwa nchi hiyo ambayo ni moja ya nchi maskini zaidi duniani.
Rais wakati huo akiwa Bingu wa Mutharika aliwasamehe wanaume hao kwa misingi ya kibininadamu ingawa alisisitiza kuwa ni kinyume na maadili ,na hata tamaduni za kiafrika na sheria za nchi.
Hata hivyo rais Joyce Banda aliyemrithi Bingu amewaambia wabunge kwamba anataka kubatilisha sheria hiyo na kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.

No comments:

Post a Comment