ILICHOKISEMA TFF NA SIMBA KUHUSU GOLIKIPA KASEJA
Katibu Mkuu wa Shirikisho Angettile Osiah |
Uongozi wa Shirikisho la soka
nchini TFF umeungana na uongozi wa klabu ya simba kwa kuwataka baadhi ya
mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuonyesha heshima dhidi ya kipa
Juma Kasseja na sio kumchukulia kama mtu wa kawaida.
Katibu mkuu wa TFF Angetille
Osiah amesema wamesikitishwa na tuhuma za wanachama na mashabiki wa
klabu ya simba ambazo zimeelekezwa kwa kipa huyo baada ya club yake
kufungwa 2- 0 na Mtibwa Morogoro.
Baadhi ya mashabiki wa Simba
walioandamana mpaka kwenye makao makuu ya Club hiyo walisema kipa huyo
ambae wanadai kiwango chake kimeshuka, anazo tuhuma pia kwamba anapokea
rushwa ili kuachia magoli.
Namkariri Angetille akisema
“nimesikitishwa na baadhi ya maneno ambayo anashutumiwa kipa Kaseja, kwa
kweli inasikitisha kwa kipa kama yule ambae ameitumikia Simba kwa muda
mrefu ameiletea mafanikio makubwa, kumrushia maneno mabaya ambayo kwa
kweli yatamkatisha tamaa, ameitumikia Simba kwa uaminifu kwa muda mrefu
sana na hata juzi walipokua wanaulizia kwamba ana kadi ngapi za njano
na sisi tulikua tunasikitika kwamba jamani mchezaji amechoka na yeye
anacheza kila mechi, wakati mwingine anaweza kukosea kwa sababu ya
uchovu, kila mechi anacheza yeye timu ya taifa inamtegemea yeye, tusije
tukamshutumu kwa makosa ambayo pengine yangeweza kuzuilika kama angekua
anaweza kupumzishwa na yeye”
No comments:
Post a Comment