TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, November 17, 2012

GARI LA TEVEZ LASHIKILIWA NA POLISI KWA KUSHINDWA KULIPIA LESEN
Gari ya Tevez likiondoshwa na trafiki baada ya kupigwa bao wakati akitokea mazoezini
Carlos Teves
MANCHESTER, England
Carlos Tevez alikumbana na kimbembe cha polisi usiku wa kuamkia jana baada ya kusimamishwa na kukamatwa kwa gari lake lililobebwa msobemsobe na polisi kwa kushindwa kulipia leseni yake.

Tevez alisimamishwa na 'trafiki' wakati akiendesha gari lake jipya jeupe aina ya Porsche Panamera jijini Manchester.

Hadi sasa, Tevez amekuwa akiendesha gari kwa kutumia leseni ya kimataifa, licha ya kuambiwa miezi 12 iliyopita kwamba anapaswa kulipia na kupata leseni halali ya kuendesha gari nchini Uingereza.

Straika huyo wa Argentina baadaye alilazimika kutolewa ndani ya gari hilo na kushuhudia 'mkoko' wake wa bei mbaya ukibebwa msobemsobe na 'winchi'.

Hata hivyo, polisi wa jiji la Manchester wameanza harakati za kumsaidia kukamilisha taratibu, lakini kwa sasa, gari la Tevez linaendelea kushikiliwa kwenye yadi za polisi.

Man City walipinga vikali madai kwamba Tevez alikamatwa, lakini gazeti la Sportsmail liliripoti kwamba straika huyo wa Argentina anakabiliwa na adhabu ikiwamo ya faini.

Tevez, ambaye hulipwa na Man City mshahara wa wiki wa paundi za England 200,000 (Sh. bilioni 500), ni shabiki mkubwa wa magari yaendayo kasi, hasa hili lililokamatwa la Porsche -- ambalo kulinunua lilimgharimu paundi za England 120,000 (Sh. milioni 300)

Alirejea mazoezini jana wakati akisubiri kujua kama atapewa adhabu nyingine zaidi. Wakati akirejea nyumbani kwake kutoka mazoezini, Tevez alionekana akichangamkia 'lifti' katika gari jingine aina ya Porsche.

No comments:

Post a Comment