STORI KUHUSU YANGA KUOMBA RADHI
Uongozi wa klabu ya Yanga 
umeomba radhi kwa taarifa zilizotolewa novemba   kuhusu uteuzi wa meneja
 Shaban Katwila, Afisa Mawasiliano Baraka Kizuguto, habari ambazo 
zilitolewa na Kaimu Katibu Mkuu Lawrence Mwalusako.
kwenye website yao wameandika 
kwamba Mwalusako kasema anaomba radhi kwa hali iliyojitokeza kwa sababu 
ameharakisha kutangaza uteuzi huo ambao bado ulikua haujadhibitishwa.
Amekaririwa akisema “Mtu 
anapoteuliwa kushika nafasi ya kazi, inapaswa kumpa taarifa muhusika 
baada ya hapo mnakaa mwajiri na mwajiriwa kukubaliana mazingira ya 
utendaji kazi na taratibu nyingine, hiki kitu kilikua bado hakijafanyika
 hivyo kitakapokua tayari tutawajulisha tena”
Kikao cha kamati ya utendaji 
kilikaa mwishoni mwa wiki na kupendekeza Katwila na Kizuguto kushika 
nafasi hizo, lakini taratibu za ufanyaji kazi wao zilikuwa bado 
hazijajdiliwa, hivyo hayo ndo makosa yaliyofanyika kuwatangaza rasmi 
wakati bado makubaliano hayafikiwa.

No comments:
Post a Comment