TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, November 5, 2012

CHADEMA YAPATA PIGO : VIONGOZI WAKE WAENDA JELA NI MADIWANI,MKURUGENZI NA MAKATIBU.

Mahakama ya hakimu mkazi Jijini Mwanza, imewatia hatiani viongozi watano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo madiwani wawili kwa kosa la kukaidi amri ya mahakama.
Viongozi hao ni Dan Kahungu ni diwani wa kata ya Kirumba, Joseph Manyerere wa kata ya Kato, Benson Kigaila ambaye ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na mafunzo ya Chadema Taifa , John Anajus ni Katibu wa Chadema wilaya ya Ilemela paoja na Katibu Mwenezi wa Wilaya hiyo Bw. Carlos Majura.
Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo Angelo Rumisha ndiye aliyewatia hatihani viongozi hao . 
Hata hivyo hukumu ya hadhabu hiyo haijaelezea ni ya aina gani kutokana na baadhi ya watuhumiwa kutokuwepo mahakamani hapo wakati hukumu ikisoma.

No comments:

Post a Comment