TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, November 4, 2012

HATIMAYE LIONEL MESSI  AITWA BABA KWA KUPATA MTOTO WA KIUME 
Messi akishika jezi ya Tshirt iliyoandikwa 1 Thiago namba 10 ambayo ni zawadi ya mtoto wake kwa kumuonesha furaha aliyokuwa nayo

Messi akiwa na mama toto wake aitwaye Antonella Roccuzzo

























Leo Messi amekuwa baba mapema leo (Ijumaa Novemba 2, 2012). Mtoto huyo wa kwanza wa Messi ambaye ni wa kiume aitwaye Thiago Messi, alizaliwa saa 11:15 jioni kwa saa za Hispania, kwenye Hospitali ya USP Dexeus mjini Barcelona.

Messi anayefahamika pia kwa jina la utani la 'La Pulga' hakufanya mazoezi na wenzake kwani katika mida ya kujifua yeye alikuwa kando ya mchumba wake kusubiria ujio wa mtoto wao wa kwanza. Messi ameahidi kuwa magoli atakayofunga baada ya tukio la leo atayatoa zawadi kwa mwanawe.

Muda mfupi tu baada ya kuzaliwa kwa mwanawe, straika huyo nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina alituma ujumbe ufuatao kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook: "Leo, nimekuwa mtu mwenye furaha zaidi ulimwenguni. Mwanangu amekuja duniani, asante Mungu! asante familia yangu kwa kuniunga mkono! Namtakia kheri kjila mmoja!".

Habari hizo zimetawala kwenye vyombo vya habari, hasa kwavile zilianza 'kubamba' tangu wiki iliyopita wakati iliporipotiwa kwamba Thiago Messi yuko mbioni kuzaliwa.

Wakati mashabiki wa Barça wakifurahia habari za kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza wa Messi, kocha Tito Vilanova amethibitisha kuwamo kwa straikia huyo kikosini katika mechi yao ya kesho (Jumamosi Novemba 3, 2012) dhidi ya Celta Vigo: "lakini ikiwa kila kitu kitakwenda sawa."

No comments:

Post a Comment