LADY JAY DEE KUTOA SOMO KWA WASANII CHIPUKIZI
![]()  | 
| Mkuu wa vipindi vya East Africa TV Lidya Igabaruza na Lady Jay Dee | 
Muimbaji mahiri wa kike hapa nchini Judith 
Wambura (kulia) almaarufu kwa jina la Lady Jay Dee akizungumza na waandishi wa 
habari leo katika mgahawa wake wa ‘Nyumbani Lounge’ uliopo jijini Dar es Salaam 
na kutambulisha rasmi kipindi chake kipya cha luninga kitakachoitwa‘Diary ya 
Lady Jay Dee’.
Amesema madhumuni ya kipindi hicho ni 
kuleta burudani tofauti kwa wapenzi wa muziki wake na muziki wa kizazi kipya kwa 
ujumla, vilevile kitatoa fundisho na changamoto kwa wasanii chipukizi kujua 
wasanii wakongwe wamepitia katika vikwazo gani.
Lady Jay Dee amesema kipindi hicho 
kitaonyeshwa ndani ya East Africa Television kuanzia tarehe 18 Novemba mwaka huu 
kila siku ya Jumapili.
Aidha ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa 
makampuni mbalimbali kujitokeza kushiriki katika kudhamini vipindi vinavyobuniwa 
kama hivyo ili kuweza kutoa ajira kwa wasanii na wadau wengine wa sekta ya 
muziki na burudani.

No comments:
Post a Comment